DUDE APATA AJALI LOLIONDO

STAA wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amepata ajali ya gari wakati akielekea Loliondo, Arusha kupata dawa ya kikombe inayotolewa na mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwaisapila.



Staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’

Dude ameiambia Bongowood kuwa, hivi karibuni walikuwa na gari aina ya Toyota Prado wakimpeleka mama yake kupata tiba ya ganzi mwilini ndipo tairi lilipopasuka na gari kuangukia gema.

“Ilipoteza muelekeo, likayumba lakini nashukuru Mungu hatukuumia, tukasaidiwa kunyanyua, tukaenda kupata tiba ya babu,” alisema Dude.

NA GPL

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz