hii ni nembo iliotengezwa kwa udongo
http://elkecole.com/wp-content/uploads/2012/09/view-from-hill-.jpg
hii ndio nyumba kamili kwa njee

UNATAKA KUJUA KUHUSU LULU NA MAMA KANUMBA WAMEFANYA NINI? SOMA HAPA UTAJUA KINACHOENDELEA:


Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni muigizaji maarufu wa filamu ameanza kuwa active rasmi kwenye tasnia ya filamu kama mwanzo  kwa kuanza kutengeneza films akiwa kama producer na pia muigizaji kama kawaida. Lulu kwasasa anashuti filamu ya Mapenzi Ya Mungu akiwa na Mama Kanumba, Linah na waigizaji wengineo huku yeye akiwa ndiye producer wa filamu hiyo. Huko nyuma alitengeneza filamu ya Foolish Age ambayo pia inatarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu na ilichelewa baada ya Lulu kupata misukosuko kuhusiana na kifo cha Kanumba ambapo pia ilibidi asicheze filamu kwanza baada ya kuwa segerea kwa miezi kadhaa kabla ya kupata dhamana

Ukichilia mbali hilo inadaiwa kwasasa baadhi ya waandaji wa filamu tayari wameanza kumtaka Lulu katika filamu zao baada ya kurudi rasmi kwenye game kama awali. Lulu ni muigizaji mwenye mashabiki wengi katika filamu ukiachilia kipaji chake na hivi karibuni alipata tuzo ya muigizaji bora wa kike kutoka Zanzibar International Film festival(ZIFF). Hivyo wapenzi wa Lulu kaeni mkao wa kula kuona cheche zake on screen kama kawaida.





Chuo kilichopo mji wa Nsuka kimeshuhudia tena mauaji ya kikatili ya dereva wa tipa ambae amewapa mimba mjane na mtoto wake. Ripoti inasema dereva huyo amechomwa moto na mtoto wa kiume wa mjane huyo,Sunday Ugwoke.

 Kutokana na habari zilizokusanywa  Sylvester Ezema alikuwa amejishikiza kwenye kampuni ya Ferguso Nig. Limited huko Akpa Edem na alikokuwa anaishi  alikuwa anashea fensi ya kawaida tu na mpenzi wake mjane. Taarifa zinasema kuwa alikuwa pia na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa kike wa mjane huyo ambaye alikuwa hajui mpaka alipofariki siku chache zilizopita ndipo alipokuja kujua.

Sylvester alichomwa moto mpaka akafa na Sunday ambaye alishamwonya aachane na mama yake na aache kufanya nae mapenzi kwenye chumba cha marehemu baba yake,ambacho kimepakana na chumba chake,Onyo ambalo marehemu Sylvester hakulizingatia na kuendelea na tendo hilo baya.
Sylvester aliyapa kisogo maonyo ya Sunday akisema kuwa huyo mjane ni 'family friend' so hakuna atakayewashitukia. Kwa kutofuata maonyo,siku moja Sunday,alijikoki na pilipili ya kusagwa na petrol akamvamia yule 'lover boy'. Sylvester alipotoka tu mlangoni kwake, Sunday alimmwagia pilipili na petrol kisha akamuwasha  moto.

Maiduguri ni moja ya majimbo yaliyowekewa sheria ya hali ya hatari

 
Takriban waumini 44 wameuawa kwa kupigwa risasi wakiwa msikitini Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa maafisa wa jimbo la Borno.
Mauaji hayo yalifanyika wakati wa maombi ya asubuhi Jumapili , ingawa taarifa zimejitokeza Jumatatu , kutokana na hitilafu ya mawasiliano kwani jimbo hilo liko chini ya sheria ya hali ya hatari.

Shambulizi lilifanyika katika mji wa Konduga, ulio umbali wa kilomita 35 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo , Maiduguri.
Washambulizi wanasemekana kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji la Boko Haram, ambalo liliwaua maelfu ya watu tangu mwaka 2009.
Gazeti la Daily Post, liliripoti kuwa watu wengine 26 walikuwa wanatibiwa kwa majeraha waliyopata wakati wa shambulizi hilo hospitalini Maiduguri.
Mwanachama wa kikundi cha vijana kinachotoa ulinzi kwa raia, aliambia shirika la habari la Associated Press, kuwa wapiganaji wao wannne waliuawa walipojaribu kutoa kilio cha kutaka usaidizi.
Raia wengine kumi na wawili, waliuawa katika kijiji cha Ngom kinachopakana na Maiduguri.
Rais Goodluck Jonathan alitangaza sheria ya hali ya hatari katika majimbo matatu Kaskazini Mashariki mwa nchi mnamo mwezi Mei wakati wanajeshi walipofanya operesheni dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Boko Haram linapigania eneo la Kaskazini mwa nchi likitaka kujitawala kwa kutumia sheria za kiisilamu.
Mwandishi wa BBC mjini Lagos, anasema kuwa wakati kundi hilo limekuwa likishambulia makanisa, pia limekuwa likishambulia misikiti.
Habari za mashambulizi hayo zilijitokeza wakati kanda ya video ya kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, ilipotolewa akidai kundi hilo kuhusika na mashambulizi hayo ikiwemo kushambulizi dhidi ya vituo vya polisi na kambi za jeshi.

clip_image001


Mtoto mmoja nchini Urusi amewashangaza wazazi na madaktari baada ya kuanza kuzungumza dakika chache baada ya kuzaliwa. Kwa mujibu wa tovuti za nchini Urusi, mtoto huyo alianza kusema neno lake la kwanza punde baada ya kuzaliwa kwa kutamka kifasaha kwa kumuita baba yake "Baba!".
Na katika dakika chache baadae mtoto huyo aliyepewa jina la Stephan alitamka "Mama!".

Miujiza ya mtoto huyo haikuishia hapo kwani siku iliyofuatia wakati mama wa mtoto
huyo alipomwambia mtoto huyo "Baba yako anakuja hospitali" kwa mshangao mtoto huyo alijibu "Nani?, Baba?".



Mama wa mtoto huyo Lisa Bazheyeva, mwenye umri wa miaka 17 na baba wa mtoto wake Rodion Bejeev wanaishi katika jiji la Norilsk nchini humo.

Madaktari waliomsaidia mama huyo wakati wa kujifungua wamethibitisha taarifa za kuongea kwa mtoto huyo.

"Nilisikia kwa masikio yangu mtoto huyo akiongea punde tu baada ya kuzaliwa" alisema Dokta Marina Panova, na kuongeza "Sijawahi kuona kitu kama hiki katika miaka yangu 23 ya kufanya katika kliniki ya uzazi"


Jesus-Christ-Wallpapers-3
dola

Maajabu mengi sana hugundulika duniani kila siku lakini kuna kila uwezekano kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee manake Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu Kristo.
Mwanasheria huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Mwanasheria huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia yoyote ya kustahili adhabu hiyo .
Dola Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua Bwana Yesu .



Msanii mkongwe  kwenye  soko  la  filamu  Tanzania,Yvonne Cherry "Monalisa"  amesema  hatarajii  kuolewa  tena  baada  ya  kuvunjika  kwa  ndoa  zake  kadhaa  ikiwemo  ile  ya  producer  Tyson....

Akisimulia  mikasa  ya  maisha  yake  mbele  ya   mwandishi  wetu,Monalisa  aliema  kuna  siku  walipokuwa  kwenye  kikao  cha  sendoff  ya  mama  yake, alitania  na  kusema  ataolewa  disemba  lakini  hakuwa  serious....

"Sina  mpango  wa  kuolewa  kabisa,kwanza  sina  mchumba, ntaolewaje?

"Siku  ile  nilikuwa  natania  tu kwa  sababu  sipo  tayari  kuolewa  na  kuachika  tena"..Alisema  Monalisa
SOURCE MAN ALONY BLOG
Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz