Wakazi waishio katika kata ya olasiti jijini arusha wameipongeza manispaa ya jiji hilo  kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa  kudhibiti utupaji wa taka ovyo  katika maeneo ya makazi wanapo ishi

Hayo yamesemwa na mmoja  wa wakazi hao akifaamika kwa majina ya Jacob marugas alipozungumza na waandishi wa habari kujua mafanikio yaliofikiwa na manispaa ya jiji hilo katika swala la usafi wa mazingira na kujionea mabadiliko makubwa tofauti nahapo awali

Pia ameongeza kuwa swla la magari kupita kila ijumaa saa nne ni tatizo hivyo ombi ni kuongezwa kwa magari nay awe ni yakupita angalau mara tatu katika wiki  ili kuepusha tatizo la uchafu kukaa kwa mda mrefu

Hata hivyo wito wake kwa serekali ni manispaa  ya jiji la arusha kuongeza idadi ya magari  ya kubebea taka  pamoja na vitendea kazi kwa wafanya kazi  pia ameitaka manispaa hiyo kupanga utaratibu mzuri wa kuwa ni sehemu gani maalumu ya wakzi kukusanya taka ili kuepuka usumbufu wa magari kushindwa kuingia









Wakazi wananao ishi  eneo la kwa morombo jijini arusha wako hatarini kukumbwa na na magonjwa ya milipuko kutokana na kutumia maji yasio sala ma
Msemaji ambae pia ni mwenyekiti wa kata orkarian bwana lairumbe mmuru  ameiomba serikali kuitazama kwa mara nyingine kwani tatizi hili limekuwa sugu na wasipo litatua magonjwa ya milipuko yapo njiani kulikumba eneo hilo kwani watu hutumia maji hayo kwa kunywa na visima sio salama
Pia ametaja maeneo yalioathirika zaidi kuwa ni  misikiti miwili, kwa morombo sokoni ,machwa, na maeneo ya dampo la kwa mrombo

wanatabora ndo 2natoka fiesta time hizi! But kitendo ambacho clouds wamemfanyia Diamond (cha kumzimia mziki mara mbili akiwa stajini) co kizuri kabisa! Kwani mchana wamem2mia vizuri katika mkutan wa fulsa lakini usiku ndo wakaamua kumzingua. Hv nyie clouds kama hamtaki msanii apaform ktk shoo zenu ni bora msimpe mualiko, kwakweli Nyie ndio mnaoua mziki wa bongo fleva. Mwanzo niliona kama JD anawasingizia but kwa mlichokifanya leo, kimedhihirisha kuwa nyie ndiyo SUMU ya bongo fleva. Halafu bila hata aibu B12 anaanza kumnanga mwenzie eti oooh! Hatutaki utozi mara nini... Honestly watanzania tunajua kuwa nyie ni redio ya burudani, but kwa mwendo huu mtageuka redio ya kuua burudani, japo mlitaka kumfanyia unaaa hata Gadzilla hilo naliacha. But co ishu mmewaboa mashabiki na pia mmefanikisha juhudi zenu za kumdhalilisha Platnumz..
NB: KIPAJI HUTOLEWA NA MUNGU NA SIYO NYIE CLOUDS HIVYO MSIWANYANYASE WASANII KIIVO, NA BINAFSI SIJUI KAMA NYIE NDO MGEPEWA NAFASI YA KUGAWA VIPAJI, NINA MASHAKA NA MGAO WENU AMBAVYO UNGEKUWA. Duh mi nilidhania ni kina Ruge na Kusaga 2 kumbe hata Dj Zero n' B12. Ushauri: nyie baadh ya wafanyakazi wa clouds fm acheni roho za ivo ili 2jenge na 2kuze Mziki we2 wa bongo.
Credit:Mdau

NI matumaini yangu muwazima na mko na hamu kubwa ya kujua kile ambacho nimewaandalia kwa siku ya leo. Kama kawaida sitatoka nje ya mapenzi. Nitazungumzia mapenzi kila siku kwa kuwa najua yanachukua sehemu kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku.

Mapenzi huweza kumfanya mtu akaishi maisha ya raha mustarehe hasa pale anapompata mtu mwenye penzi la kweli lakini pia usipoyajulia mapenzi yanaweza kukutoa roho.
Wangapi leo hii wamechanganyikiwa kutokana na kukataliwa penzi na watu waliotokea kuwapenda? Wangapi wamejiua baada ya kuachwa na wapenzi wao? Wangapi wanashindwa kufanya kazi zao kwa ufasaha kwa sababu wamekorofishwa na wapenzi wao?
Hakika ni wengi na kwa maana hiyo basi kama unataka kuishi maisha ya raha, pamoja na mambo mengine hakikisha huchezi kamari kwenye mapenzi, ingia katika uhusiano unaofaa ili mwisho wa siku furaha ichukue nafasi katika kila siku iendayo kwa Mungu.
Wiki hii naomba nizungumzie swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza bila kupata majibu sahihi kiasi cha kuwafanya washindwe kuishi maisha ya furaha na wapenzi wao. ‘Hivi mpenzi wangu ananipenda kwa dhati?’ Hili ni swali wanalojiuliza wengi walio katika uhusiano.
Huenda hata wewe ulishawahi kujiuliza swali hili na mpaka sasa hujabaini ukweli wa penzi lake kwako na kama hujawahi kujiuliza swali hili basi hauko makini katika uhusiano wako. Hivi wewe ambaye unajiamini kwamba mpenzi wako anakupenda, kuna vigezo gani ambavyo vinakudhihirishia hilo?
Labda niseme tu kwamba, mapenzi ya sasa yamejaa usanii wa hali ya juu sana. Unaweza ukajikuta uko na mpenzi ambaye anaonesha kukupenda, kukujali na kukuheshimu sana kiasi cha kukufanya uamini kwamba anakupenda kutoka moyoni mwake lakini kumbe anajifanyisha.
Yaani huo ndiyo ukweli wenyewe na usishangae hata huyo uliyenaye akawa anakupotezea muda wako tu. Unachotakiwa kukifanya ni kumfanyia uchunguzi wa kina kubaini ukweli wa penzi lake kwako.
Sawa huwezi kufunua moyo wake na kuangalia kama kweli anakupenda lakini kuna vitu vidogo vidogo vinavyoweza kukusaidia kumbaini mtu mwenye penzi la kilaghai.

Ni rahisi kumbaini?
Niseme tu kwamba hakuna mtu anayeweza kuwa na uhakika wa asilimia mia moja kuwa mpenzi wake anampenda kwa dhati na kama unaamini hivyo, unajidanganya. Hii ni siri ya mwenye kupenda na ndiyo maana unaweza kukuta mpenzi wako anakusisitizia kwamba anakupenda lakini bado unashindwa kuamini.
Wataalam wa masuala ya mapenzi wanasema, kumdhihirishia mpenzi wako kwamba unampenda siyo lazima umwambie NAKUPENDA! Vitendo vyako ndivyo vitamfanya aamini hivyo.

Asiyekupenda utamjua tu  
Hukatazwi kumpenda mtu lakini bahati mbaya inakuwa pale utakapotokea kumpenda mtu asiyekupenda na akajilazimisha kukupenda ili kukuridhisha.
Walio katika aina hii ya mapenzi wako wengi. Mtu anaona kabisa mwanaume anamnyanyasa, anampiga, anamtukana, anamdhihaki, hamuoneshi kumpenda kwa dhati, hamjali lakini mwanamke anamng’ang’ania tu eti kwa sababu anampemnda sana.
Hivi mwanamke kama huyu anashindwa kubaini kuwa mwanaume aliyenaye hana penzi la dhati kwake?
Ifike wakati basi ukae chini na utafakari penzi analokupa mpenzi wako na kuchukua uamuzi sahihi, kumuacha au kuendelea naye. Usikubali hata siku moja kupotezewa wakati na mtu asiyelithamini penzi lako.


  Maisha Tuck Shop lililopo Barabara ya Veld, Athlone, ambapo Watanzania watatu walipigwa risasi na kufariki.
Watanzania watatu waliuawa Jumanne iliyopita jijini Cape Town, Afrika ya Kusini kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Watanzania hao walipigwa risasi na kundi la watu waliokuwa wameficha nyuso zao nje ya duka lijulikano kama Maisha Tuck Shop lililopo katika barabara ya Veld katika kitongoji cha Athlone, jijini Cape Town.

Watanzania wawili walifariki hapo hapo na mmoja alifariki baada ya kufikishwa hosipitali. Mwanamke mmoja, raia wa Afrika Kusini, alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo. Mmiliki wa duka hilo, Ashim Nassoro, alisema kuwa aliona kundi la watu wakiwa na bunduki za aina ya AK-47 na pistols wakipiga risasi nje ya duka lake.

Bw. Nassoro alisema amesikitika sana na shambulio tukio hilo na kudai waliouawa walikuwa marafiki zake. Alisema yeye alikuwa ndani ya nyumba, ambayo iko karibu na duka hilo pamoja na mke wake na mtoto wake wa miaka mitatu wakati milio ya risasi ilipoanza.

“Nilikuwa ndani na nilimwambia mke na mtoto wangu walale chini mpaka milio ya risasi iishe” alisema Nassoro na kuongeza “waliwapiga risasi watu waliokuwa ndani ya nyumba halafu wakaenda kwenye duka. Walikuwapiga risasi watu wawili dukani, mmoja aliyekuwa kwenye geti na mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye nyumba.”

Nasoro aliongeza kuwa alikuwa anawajuwa Watanzania hao kwa sababu wote wanatoka Tanzania na wamekuwa wakiishi pamoja tokea walipowasili Cape Town miaka mitano iliyopita. Mtu mwingine aliyeshughudia tukio hilo alisema kuwa waliowauwa Watanzania hao walikuwa hawana wasiwasi na walirudi kwenye gari yao taratibu na kuondoka eneo la tukio.

Kufuatia tukio hilo, polisi ilimkamata Abdus Salaam Ebrahim ambaye ni kiongozi wa kikundi kinachopiga vita dhidi ya uhalifu na madawa ya kulevya nchini humo kinachojulikana kama People Against Gangsterism and Drugs (Pagad). Abdus Salaam Ebrahim amefikishwa mahakami leo kwa mashtaka ya mauaji.

Hata hivyo, mahakama imeyaondoa mashtaka hayo kwa muda kufuatia ombi la mwendesha mashtaka ili kuruhusu uchunguzi zaidi kufanyika. Wakati hakimu akiyandoa mashtaka hayo, wafuasi wa kikundi hicho cha Pagad waliokuwa wamejazana mahakamani hapo walishangilia huku wakisema “Allahu Akbar”. Majina ya Watanzania waliouawa hayakuwekwa kwenye charge sheet.

Pagad ni kikundi kilichoanziswa mwaka 1995 kupambana na uhalifu na madawa ya kulevya kwenye jiji la Cape Town baada baada ya juhudi za serikali kulegalega. Kampeni ya kikundi hiki ilianza mwaka 1996 baada kumkamata, kumpiga na kumchoma moto hadi kufa Rashaad Staggie ambaye alikuwa kiongozi wa kikundi cha uhalifu jijini Cape Town. Serikali ya Afrika Kusini ilishawahi kudai huko nyuma kuwa Pagad ni kikundi cha kigaidi baada ya kudaiwa kulipua kwa bomu hoteli ya Planet Hollywood mwaka 1998. Hata hivyo, Pagad ilipinga kuhusika kwenye shambulio hilo.

Kikundi hiki kilipotea lakini kikaja kuibuka tena kuanzia mwaka 2011 na kampeni yake ya kuchukua mitaa inayotawaliwa na uhalifu na biashara ya madawa ya kulevya. Wadadisi wa mambo wanadai kuwa kurudi tena kwa Pagad kwa gia ya kupambana na uhalifu, hasa madawa ya kulevya, itafanya hali kuwa mbaya hasa kwenye jimbo la Western Cape.

Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la milipuko ya mabomu kwenye sehemu zinazouza magari na pia kwenye nyumba za makazi ya watu zilizopo Athlone na maeneo mengine jijini Cape Town. Matukio haya yamekuwa yakitokea zaidi kwenye nyuma za makazi zinazotuhumiwa kutumika kufanyia biashara ya madawa ya kulevya. Kikundi cha Pagad kimekanusha kujihusisha na matukio hayo.
Source:- JF Blog


Stori: Mwandishi Wetu
Hakika aliyemmwagia tindikali bilionea Said Mohamed Saad, alifanya kitendo kibaya kupitiliza, kwani athari ambazo amemsababishia ni kubwa kiasi ambacho hata upatikanaji wa tiba mahsusi umekuwa wa kutangatanga.

Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali bilionea Said Mohamed Saad hospitalini.

Gazeti hili linazo taarifa za ndani na zenye uhakika kuwa Said ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Home Shopping Centre, amekimbizwa Ujerumani kwa matibabu zaidi baada ya kushindikana Afrika Kusini alikopelekwa awali.

Said alimwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu, mishale ya saa 2 usiku akiwa kwenye moja ya maduka yake yaliyopo kwenye jengo analodaiwa kulimiliki la Msasani Mall.

Ilielezwa kuwa baada ya kumwagiwa tindikali, alikimbizwa kwenye Hospitali ya Ami Wellness Centre iliyopo Masaki, Dar es Salaam lakini ndani ya kipindi kisichozidi dakika 60, alichukuliwa na kupandishwa ndege kupelekwa Afrika Kusini.

Said Mohamed Saad akiwa hospitali.

AFRIKA KUSINI MATUMAINI KIDOGO
Ndugu wa Said aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, alisema kuwa akiwa Afrika Kusini, ilionekana kwamba bilionea huyo anatakiwa kufanyiwa oparesheni ya uso ili kuondoa ngozi iliyoathiriwa na tindikali, vilevile kulifanyia jicho upasuaji.
“Sehemu ya usoni kushuka kifuani upande wa kulia na mkono wenyewe wa kulia ndiyo maeneo katika mwili wa ndugu yetu yaliyoathirika zaidi na tindikali,” alisema ndugu huyo wa ndani kabisa kwa sharti la kutotajwa jina na kuongeza:

“Jicho la kulia lenyewe limepata athari kidogo, kwani inaonekana wakati mmwagaji akifanya kile kitendo, yeye alifumba macho kwa hiyo tindikali haikuingia ndani ya jicho, iliishia kwa juu.
“Ila kwa vile tindikali ilimwagika kwa wingi juu kwenye jicho la kulia na kutokana na ukali wa tindikali aliyomwagiwa, imesababisha kutengenezwa kwa mtoto wa jicho kwa hiyo hawezi kuona mbali.

“Uamuzi wa kumpeleka Ujerumani uliafikiwa baada ya kujiridhisha kwamba kule kuna wataalamu kuliko Afrika Kusini. Oparesheni ya uso kubadili ngozi iliyoathirika, vilevile kufanya upasuaji wa jicho na kuliweka sawa ni mambo ambayo tulijiridhisha yanawezekana Ujerumani.”

AKATAA KUTAJA JINA LA HOSPITALI
Kwa mujibu wa ndugu huyo, Said aliondolewa Afrika Kusini na kupelekwa Ujerumani, Agosti 3, mwaka huu na tangu hapo taarifa zake zimefanywa siri kubwa ili kulinda usalama wake.
“Hata wakati nazungumza na wewe kama mwandishi wa habari, nilijua tu lazima utaniuliza kuhusu jina la hospitali aliyolazwa Ujerumani. Ukweli ni kwamba siwezi kukwambia. Tunafanya hivyo kwa ajili ya usalama wa ndugu yetu.

“Tukio la kumwagiwa tindikali ni zito sana, imeshajionesha wazi namna ambavyo kuna watu hawampendi, hao maadui wakijua hospitali aliyolazwa, wanaweza kufanya juu chini wamfikie na kumdhuru kwa mara nyingine. Hilo jambo hatutaki kabisa litokee,” alisema ndugu huyo.

NDUGU, WATOTO WAKE WAZUIWA KWENDA UJERUMANI
Habari zaidi zinabainisha kuwa ndugu wa Said walipanga kwenda Ujerumani kumtembelea lakini walizuiwa kwa sababu awamu hii, viongozi wa familia yake wamezingatia usiri.
“Kuna watoto wake walikwenda Afrika Kusini na walikuwepo wakati anasafirishwa kwenda Ujerumani lakini waliambiwa warudi Tanzania kwa sababu kule Ujerumani utaratibu umebadilika. Watu wachache wanaohusika na huduma pamoja na usalama wake ndiyo pekee wanaoruhusiwa,” alisema, akaongeza:

“Wapo ndugu wengine kutoka Saudi Arabia na Oman, vilevile nao wamezuiwa kwenda Ujerumani kumwona. Ni katika kuhakikisha mambo hayawi kama ilivyokuwa Afrika Kusini, maana kule ilishakuwa hatari, ndugu wengine wanaingia wodini, wanampiga picha na kusambaza mitandaoni. Safari hii mambo hayo hayatakiwi.”

APELEKWA UJERUMANI BAADA YA JK
Imeelezwa kwamba Said alipelekwa Ujerumani wiki moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete kwenda kumtembelea alipokuwa amelazwa kwenye hospitali moja nchini Afrika Kusini.
Dk. Kikwete, alikuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini alipokwenda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya Afrika (SADC), kuhusu pande tatu za umoja huo (Troika of SADC), hivyo kupata fursa ya kwenda kumjulia hali.

MUNGU AMPONYE SAID
Dawati la gazeti hili linamuombea Said apone kwani alionesha moyo wa ukarimu kwa familia 655 zilizokumbwa na mafuriko eneo la Jangwani, Desemba, 2011 kisha kuhamishiwa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

MTUHUMIWA BADO KUKAMATWA
Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura alisema kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya kazi kwa nguvu na umakini mkubwa lakini mpaka sasa halijafanikiwa kumpata mtuhumiwa.

GPL

MWANAMKE mmoja ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyankumbu, Kata ya Kalangalala mkoani  Geita amenusurika kifo baada ya kujimwagia mwilini mafuta ya petroli kisha kujilipua baada ya mumewe kuoa mke wa pili.  
Imeelezwa kuwa mwanamke huyo, Anastazia Kubezya (28) Agosti 8 mwaka huu aliamua kujimiminia petroli mwili mzima kabla ya kuchukua kiberiti na kujilipua, hali iliyosababisha  akimbizwe katika Hospitali ya Geita alikolazwa katika wodi namba saba kwa matibabu.
Akizungumza na gazeti hili, Consolata Raphael ambaye ni dada wa majeruhi huyo alidai kuwa chanzo cha mdogo wake huyo kufikia hatua ya kutaka kutumia njia hiyo ya mkato kwa lengo la kujiua ni wivu wa mapenzi.



Consolata alisema: “Siku ya tukio shemeji yangu George Kubezya (mume wa majeruhi), alifika nyumbani kwa mdogo wangu wa kiume akidai kuwa mkewe huyo anatishia kujiua baada ya kuoa mke wa pili. “Tukiwa tunaendelea kujadiliana mara alitokea mkewe Kubezya akiwa na viatu vya mwanaye mdogo akamkabidhi mdogo wetu mwingine aitwaye Rozalia akamwambia mpatie mwanaye kwa kuwa anaondoka na hajui atarudi lini.
“Baada ya kutamka maneno hayo aliondoka na niliwasiliana na ndugu yetu mwingine aitwaye Elizabeth aliyesema Anastanzia alipita kwake akiwa na chupa ikiwa na petroli na walipojaribu kumkimbiza alipotelea gizani.

“Kati ya saa 4 na saa 5 usiku Eliza na wenzake walisikia mtu akilia nje ya nyuma yao na baada ya kutoka nje walikuta Anastanzia akiwa tayari amekwisha jilipua moto, walipomhoji alidai amefanya hivyo ili afe kutokana na mumewe kumuolea mke mwenza na kumleta kwenye nyumba waliyoijenga yeye na mumewe,”alisema Consolata.

Hata hivyo juhudi za kumpata mumewe kuzungumzia sakata hilo hazikuzaa matunda baada ya kile kilichoelezwa kuwa alitoroka muda mfupi baada ya kumfikisha mkewe hospitalini.



Gazeti hili lilifika hospitalini hapo na kukuta mwanamke huyo aliyelazwa wodi namba nane akiwa anauguzwa chini ya ulinzi wa polisi ili akipona afikishwe mahakamani kwa kosa la kujaribu kujiua.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dk. Adam Sijaona akizungumzia hali ya majeruhi huyo alisema bado si nzuri na wanafanya mpango wa kumhamishia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.
Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz