Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akizindua rasmi gari ya Nissan Patrol aina ya Y62 leo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo wa gari hiyo mpya ambayo ni Four Wheel Drive yenye uwezo wa kubeba watu 8 na yenye nguvu ya 5.6L V8 injini yenye spidi ya 240 ni ya pekee duniani kuzinduliwa na Tanzania inakuwa ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na kati kuingia baada ya Congo DRC, Angola na Ghana.
Bw. Mcintosh amesisitiza kwamba gari hii inaviburudisho pamoja na Tv katika hali ya kumsaidia dereva kwenye safari ndefu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya CFAO Motors na wageni waalikwa wakimsikiliza Bw. Wayne Mcintosh (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors Tharaia Ahmed (wa pili kulia) na baadhi ya wageni waalikwa.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akiendesha bahati nasibu ya kwenda kushuhudia fainali na Michuano ya kombe la Mataifa barani Afrika inayofanyika nchini Afrika kusini kwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akitangaza washindi wawili watakaoenda nchini Afrika Kusini kushuhudia fainali za mashindano ya AFCON.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akimpongeza mshindi wa shindano la bahati nasibu Group Manager wa DELFINA Bw. Sajjad Dharamsi atakayeenda nchini Afrika Kusini kushuhudia fainali za mashindano ya michuano ya AFCON 2013. Kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
Bw. Wayne Mcintosh akimpongeza mshindi wa pili wa Kampuni ya Wambi Lube Oil Distributor Bw. Omari Omari.
Peer Educator wa CFAO Motors Maria Petro (kulia) akimpongeza Bw. Omari Omari kwa kushinda droo ya kwenda kutizama fainali za AFCON 2013 nchini Afrika Kusini iliyoendeshwa na kampuni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari mpya aina ya Nissan Patrol Y62. Katikati ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
Afisa Mauzo wa CFAO Motors Magdalena Mpeku akitoa maelezo ya gari mpya aina ya Nissan Patrol Y62 kwa baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akizungumza na mmoja wa wateja wakati wa uzinduzi wa gari aina ya Nissan Patrol Y62 makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar.
Wageni waalikwa wakila na kunywa wakati wa hafla hiyo.
Warembo waliokuwa wakikaribisha wageni wakipozi kwenye gari hiyo mpya aina ya Nissan Patrol Y62.


Ulinzi Shirikishi
Wananchi mkoani Arusha wametakiwa kuwa na uhuru wa kuteuwa na kawatumbua watu wanatakiwa kufanya doria ya ulinzi shirikishi katika mitaa yao nyakati za usiku.
Akuzungumza na waandishi wa habari msaidizi wa mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha Ndg.Yona Maziba amesema kuwa ili kuepukan na makundi ya watu wanaoigiza kuwa ni polisi jamii na kumbe ni vibaka wanaotumia fursa hiyo kuwateka wakazi wa mtaa husika na kuwachukulia vitu vyao pindi wanapo nyumbani nyakati za usiku.
Amesema pamoja na kutoa semina kwa makamanda waandamizi wa ulinzi shirikishi lakini bado wanakabiliwa na makundi yasiyo sahihi na teule kwa kufanya shughuli hiyo na ndiyo maana hali hiyo inawawia vigumu wao wenye kutambua ni makundi ya aina gani yanajishughulisha na utekaji na kuigiza wao kama polisi jamii.
Pia ameongeza kuwa kila mwananchi anatakiwa kuwa na uhuru wa kuhoji makundi ya namna hiyo kuwa kama wana vitambulisho vyenye kuonyeasha wao ni akina nani kwani huwa kuna mavazi maalumu wanayovaa kwaajili ya lindo.
Kamanda Yona ameongeza kuwa uzalendo ni fursa yetu binafsi hivyo katika hilo inahitajika wananchi kuwa wazalendo kwani unapo kuwa mzalendo na nchi pia hata na mtaa wakon ni dhahiri kuwa utajilinda na kuulinda mtaa wako na nchi yako kwa ujumla kwa kufichua watu wanaojihusisha na tabia hizo za utekaji na uporaji wa mali za watu ili waweze kufikishwa mahali husika na kupewa adhabu stahiki .

Wananchi mkoani Arusha wametakiwa kuwa na uhuru wa kuteuwa na kawatumbua watu wanatakiwa kufanya doria ya ulinzi shirikishi katika mitaa yao nyakati za usiku.
Akuzungumza na waandishi wa habari msaidizi wa mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha Ndg.Yona Maziba amesema kuwa ili kuepukan na makundi ya watu wanaoigiza kuwa ni polisi jamii na kumbe ni vibaka wanaotumia fursa hiyo kuwateka wakazi wa mtaa husika na kuwachukulia vitu vyao pindi wanapo nyumbani nyakati za usiku.
Amesema pamoja na kutoa semina kwa makamanda waandamizi wa ulinzi shirikishi lakini bado wanakabiliwa na makundi yasiyo sahihi na teule kwa kufanya shughuli hiyo na ndiyo maana hali hiyo inawawia vigumu wao wenye kutambua ni makundi ya aina gani yanajishughulisha na utekaji na kuigiza wao kama polisi jamii.
Pia ameongeza kuwa kila mwananchi anatakiwa kuwa na uhuru wa kuhoji makundi ya namna hiyo kuwa kama wana vitambulisho vyenye kuonyeasha wao ni akina nani kwani huwa kuna mavazi maalumu wanayovaa kwaajili ya lindo.
Kamanda Yona ameongeza kuwa uzalendo ni fursa yetu binafsi hivyo katika hilo inahitajika wananchi kuwa wazalendo kwani unapo kuwa mzalendo na nchi pia hata na mtaa wakon ni dhahiri kuwa utajilinda na kuulinda mtaa wako na nchi yako kwa ujumla kwa kufichua watu wanaojihusisha na tabia hizo za utekaji na uporaji wa mali za watu ili waweze kufikishwa mahali husika na kupewa adhabu stahiki.

Wanjeshi kutoka Chad walioingia mjini Kidal kusaidiana na jeshi la Ufaransa
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, ameelezea kile anachosema ni vita vya kweli vinavyoendelea nchini Mali baada ya makabiliano mapya kutokea karibu na mji muhimu Kaskazini mwa nchi.
Alisema kuwa wanajeshi wa Ufaransa wamepigana kile walichotaja kuwa wafuasi wa makundi hayo ya wapiganaji wanaopigana viungani mwa mji wa Gao
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kuwa aliweza kusikia sauti za milipuko.
Mji wa Gao ulikuwa ngome ya wapiganaji hao lakini maafisa wa Ufaransa walitangaza kuwa majeshi yaliweza kukomboa mji huo.
Wakati huohuo,mamia ya wapiganaji wa kiisilamu wameuawa nchini Mali tangu majeshi ya Ufaransa kuanza kupambana nao mwei jana.
Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, wengi waliuawa katika mashambulizi ya angani pamoja na makabiliano ya moja kwa moja na wanajeshi wa Ufaransa.
Wananchi wa Mali wamepata afueni baada ya wapiganaji
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje Laurent Fabius, amesema kuwa Ufaransa huenda ikaanza kuondoa wanajeshi wake Mali kuanzia mapema mwezi Machi.
Kwenye mahojiano kupitia kwa vyombo vya habari,alisema kuwa ikiwa kila kitu kitakwenda sawa, idadi ya majeshi huenda ikapungua.
Ufaransa ina takriban wanajeshi 4,000 nchini Mali. Hapo jana mkutano wa maafisa kutoka UN, EU na Afrika ulianza mjini Brussels kujadili hatua zitakazochukuliwa baada ya wanjeshi wa Ufaransa kumaliza kazi yao.
Aidha waziri wa ulinzi alisema kuwa mji uliokuwa umesalia kuwa chini ya waasi ,Kidal, tayari umedhibitiwa na majeshi ya Ufaransa.
Maeneo ya milimani ambako wapiganaji wanajificha
Mashambulizi ya angani dhidi ya waasi yanaendelea katika maficho yao kaskazini mwa nchi.
Bwana Le Drien alisema kuwa wapiganaji hao walifariki katika mashambulizi ya angani, wengine waliuawa wakiwa kwenye magari yao, na wengine katika mashambulizi ya ardhini mjini Konna mwanzoni mwa kampeini ya kupambana na nao.
Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz