-
STAA WA MUZIKI NCHINI NIGERIA 2FACE IDIBIA AFANYA ARUSI KIMILA NA HIZI NI BAADHI TU YA PICHA ZAKE
TAARIFA KUHUSU HUKUMU ALIYOHUKUMIWA MMILIKI WA CLUB YA AC MILAN.
Mmiliki wa club ya soka ya AC
Milan ya Italia Silvio Berlusconi ambae pia aliwahi kuwa waziri mkuu wa
nchi hiyo, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kukutwa
na hatia ya kuingilia mawasiliano ya simu ya mpinzani wake wa kisiasa
pasipo kuwa na kibali.
Hii ni adhabu ya pili ya kifungo ambayo imempata Berlusconi baada ya ile ya kashfa ya fedha zisizo halali za kampuni yake ya filamu ambapo zaidi ya hapo anazo kesi nyingine mbili ikiwemo ya kufanya mapenzi na binti mwenye umri wa miaka 17, na pia kukwepa kulipa kodi
Hii ni adhabu ya pili ya kifungo ambayo imempata Berlusconi baada ya ile ya kashfa ya fedha zisizo halali za kampuni yake ya filamu ambapo zaidi ya hapo anazo kesi nyingine mbili ikiwemo ya kufanya mapenzi na binti mwenye umri wa miaka 17, na pia kukwepa kulipa kodi
Uhuru Kenyatta ndiye Rais mpya wa Kenya
Uhuru Kenyatta ndiye Rais wa nne
wa Jamuhuri ya Kenya baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza kushinda
uchaguzi wa kihistoria wa Kenya.
Ni baada ya siku tano tangu wakenya kupiga kura
kuwachagua rais, magavana, maseneta , waakilishi wa bunge, waakislihi
wanawake na waakilishi wa wodi.Uhuru alipata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizohitajika ili kupata ushindi kulingana na mahitaji ya katiba mpya ya nchi.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa Uhuru Kenyatta ameshinda na hivyo kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Tume ya uchaguzi ilichukua zaidi ya masaa matano kukagua hesabu ya kura hizo kabla ya kutangaza matokeo hii leo siku tano baada yawakenya kupiga kura.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Awali duru zilisema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho
Subscribe to:
Posts (Atom)
0 comments: