Chadema yawataja 10 utekaji Kibanda

Waenda mahakamani leo kuomba simu zao hadharani.

                Wamo wana usalama, waandishi wa habari na wanasiasa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibua mapya katika sakata la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, kwa kuwataja watu 10 waliodai kuwa ni wahusika wa matukio ya ugaidi nchini.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu njama za kuichafua Chadema zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyombo vya dola ukiwamo Usalama wa Taifa.

Marando ambaye alisema kuwa amepata taarifa hizo kutokana na ujuzi wake kama mwansheria na mtu ambaye amepata ujuzi wa kazi za ushushu, hivyo alifanya uchunguzi wa matukio hayo ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi.

Waliotajwa kuhusika na matukio hayo ni pamoja na Waziri mmoja, maofisa wa Usalama wa Taifa watatu, akiwamo mmoja wa mwenye wadhifa wa juu, kada mwandamizi wa CCM, Mhariri Mtendaji mmoja wa gazeti, washitakiwa wawili wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi mahakamani, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na Ludovick Rwezahula.

Wengine ni ofisa aliyepata kufanya kazi Makao Makuu ya Chadema, Mwandishi na Mpigapicha mmoja wa magazeti ya serikali, mtoto wa kigogo serikalini na aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Stephen Ulimboka.

Marando alisema leo, ataongoza timu ya mawakili wa Chadema kwenda mahakamani kuomba maelezo ya simu zao kutaka kampuni za simu za mikononi kuwasilisha maelezo ya mawasiliano yanayodaiwa kupanga njama za ugaidi na hususani utengenezaji wa video iliyomtia matatani Lwakatare.

Kutokana na sababu mbalimbali za kitaaluma na maadili, tumeamua kusitiri majina hayo kwa sasa, licha ya kutamkwa hadharani na Marando, huku tukiendelea kukamilisha wajibu wetu wa kiuandishi kabla ya kuwataja.

Marando ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema, alisema watu hao ni muhimu sana katika upangaji wa mkakati wa utengenezaji wa video ya Lwakatare na vitendo vya kihalifu vya utekwaji wa Kibanda na tukio la kutekwa na kisha kutupwa msituni kwa Dk.  Ulimboka.

Alisema Chadema inazo taarifa kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao, kada mwandamizi wa CCM kwa sasa anafanya mipango na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni  ya simu ya Vodacom ili kumsaidia kufuta taarifa zake za mawasiliano aliyokuwa anayafanya na baadhi ya wanachama wa Chadema na maafisa usalama wa Taifa kufanikisha mkakati huo, kitu ambacho ni kinyume cha Sheria za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Alisema kada huyo na wenzake ndio waliopanga njama za utekaji wa Kibanda na wakatimiza lengo hilo.

Alisema CCM inatambua kuwa katika hali ya sasa hakiwezi kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ndiyo maana wanapanga kila mbinu chafu kuiangamiza Chadema.

Marando alisema kada huyo na wenzake walipanga kumteka Kibanda wakatimiza lengo hilo, baadaye wakaingia kwenye ‘Plan B’ ya kutaka kuihusisha Chadema kwa kumtumia Rwezahula ambaye ni mshitakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatare kufanikisha mkakati huo wa kishetani.

Alisema mwandishi na mpigapicha ni mtu muhimu sana mahakamani kwa kuwa ndiye aliyeandika ujumbe kwa njia ya barua pepe (email) kuipongeza ofisi binafsi ya Rais na Usalama wa Taifa kwa kupata video ya Lwakatare.

“Pongezi za (anamtaja mwandishi na mpiga picha huyo) kwa TISS (Idara ya Usalama wa Taifa) ndizo zinanisukuma kuiomba mahakama kuagiza kupatikana taarifa zake (anamtaja tena) anaipongeza TISS kwa kuibua njama za wahalifu, lakini mimi ninajua TISS ikipata njama za aina hiyo haraka inapeleka ushahidi polisi, lakini huu wa Lwakatare ulipelekwa YouTube badala ya kwenye vyombo vya sheria,” alisema Marando.

Alisema miongoni mwa mawasiliano hayo ni yale ya Disemba 28  mwaka jana siku ambayo mkanda wa Lwakatare umerekodiwa, Machi 4 na 6 mwaka huu ambayo ilikuwa ni siku moja kabla ya Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane wa Machi 13 mwaka huu ambako mchana uliofuata Lwakatare kukamatwa.

“Mawasiliano na (anamtaja kada mwandamzi wa CCM) na (anamtaja ofisa wa Usalama wa Taifa) katika kipindi hicho nayo tunayahitaji kwa sababu huyu (anataja jina la Ofisa Usalama wa Taifa) anayetumia simu 0754 006355 mbali na kuwasiliana na (anamtaja kada mwandamzi wa CCM) ndiye aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka Dk. Ulimboka na ndiye aliyewasialiana na (anamtaka ofisa wa zamani wa Chadema) kati ya Januari 20 na Machi 6 mwaka huu,” alisema Marando.

Marando anamtaja Ofisa Usalama wa Taifa huyo kwa jina, kuwa anafanya kazi makao makuu na ndiye anayetumika kuendesha michezo ya kuhonga wanasiasa wa CCM na upinzani, na pia anapangia wabunge mambo ya kuongea kwa maslahi ya CCM.

Marando alimtaja ofisa usalama mwingine jina tunahifadhi kuwa ndiye aliyekutana na ofisa usalama wa Chadema, (jina tunahifadhi) na wenzake Machi 29 mwaka huu katika hoteli ya Sea Clif jijini Dar es Salaam.

Alisema katika mkutano huo, Ofisa Usalama huyo alimtaka Ofisa wa Chadema akubali kutumika kwa kutoa taarifa za vikao vya chama, kuwasilisha kwake nyaraka za Kamati Kuu na kueleza mipango ya Chadema katika kesi ya Lwakatare.

“Kwenye mpango huu, afisa huyo wa Usalama wa Taifa ambaye ninamfahamu vizuri alimuahidi … (anamtaja Ofisa wa Chadema) kiasi cha Sh. milioni 30 na kwamba fedha hizo angelipwa wiki iliyopita, aliahidiwa kwamba kila nyaraka atakayopeleka atalipwa ujira na kila mwezi atakuwa analipwa Sh. 500,000,” alisema Marando.

Ofisa Usalama wa Taifa huyo alipopigiwa simu na NIPASHE alimuuliza mwandishi kama hao Chadema wamemtaja kwa jina gani na baada ya kueleza alisema jambo hilo kwake ni jipya na kwamba ndiyo kwanza analisikia.

Ofisa Usalama mwingine anayetuhumiwa alipopigiwa simu na mwandishi kujitambulisha na kumweleza madai ya Chadema alikata simu wakati simu ya Ofisa Mwandamizi wa Usalama wa Taifa, simu yake ilikuwa haipatikani.

Kada mwandamizi wa CCM ambaye amekuwa akitajwa sana katika siku za hivi karibuni, simu yake ya kwanza ilipokelewa na mtu mmoja aliyedai siyo yeye na simu ya pili ilikuwa ikiita bila kupokewa.

Waziri anayetuhumiwa simu yake ilikuwa ikiita bila kupokewa, wakati mtoto wa kigogo mmoja serikalini alipotafutwa simu zake mbili zilikuwa hazipatikani; naye aliyepata kuwa mtumishi wa Chadema Makao Makuu, alipopigiwa simu ilipokewa, lakini baada ya mwandishi kujitambulisha aliikata.

Aidha, Mhariri anayetuhumiwa simu yake iliita bila kupokewa.

Hayo yameibuka wakati wananchi wakisubiri ahadi ya polisi kwamba ukweli juu ya nani hasa anayetuhumiwa kuhusika na sakata la kutekwa na kuteswa kwa Kibanda, angejulikana leo.

Wiki iliyopita, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Issa Mngulu, alisema kuwa ripoti ya upelelezi wa timu maalum ya wapelelezi itatolewa kati ya Aprili 15, 16 au 17, mwaka huu.

0 comments:

HII NDIO LIST YA WASANII WATAKAOKUWEPO KWENYE PROJECT YA JUMA NATURE

Project zangu mpya ambazo nakuja nazo sasa hivi ni za wasanii tofauti tofauti, nimemshirikisha Tunda Man kwenye Haipotei kwasababu anakubalika katika jamii, ni msanii mpya ambae anaeleweka katika jamii, na wako wengine wengi tu ikiwa ni pamoja na Kitale, kingwendu na wengine wengi kama kina Stoppa, wapya pia ambao wanakuja sasa hivi kina Dogo Lila, mwaka huu sitegemei kutoa album wasababu soko linayumba.

Licha ya kuachia single mpya Nature pia ameachia tshirts zenye chata ya Haipotei

  Na hizi zipatakiana Mbagala Zakiem ukiuliza kwa Nature ndio zinapatikana hapo. mwanzoni nilizigawa tu lakini sasa hivi ndio tumeamua kuweka duka na zinauzwa kwa shilingi 16,000 tu..

0 comments:

DUDU BAYA ANG'AKA NA PROF: JAY NI KUHUSU RING TONES NA RINGBACK TONES

Siku moja baada ya Prof Jay kutoa maoni yake kupitia 255 ya kipindi cha XXL juu ya maswala ya Ringtones na Ringback tones,ambapo alielezea sababu za matatizo yanayoendelea katika upande wa Ringtones moja wapo ikiwa ni kutokuwepo na umoja katika wasanii wenyewe, baadhi ya mashabiki pia kwa kusapoti ngoma zisizo na maudhui mazuri ndani yake na media kupokea mizki mibovu, Dudu baya afunguka na kumuita ni mnafiki na kumfananisha na kunguru asie namabawa

"sijakubaliana na swala yeyekuzungumza sasa hivi ni mwanaharakati katika huu muziki na nna ushahidi wa kusema yeye sio mwanaharakati la pili natofautiana na yeye kusema  kwamba mziki ni big g hilo nalikataa kwasababu unavyoona vijana wa sasa hivi wanamziki kama Diamond, Ommy Dimpoz na wasanii wengine kama kina Rich mavoko, wanavyofanya wakati sisi tuhahit wanatutazama kwenye TV, na wanakuwa inspired na sisi na wanafurahia maendeleo yetu wanafurahia kushine kwetu halafu sasa hivi anasema mziki ni big g, hizo ni jelous za kichawi, na unaonyesha kwamba wewe umeshindwa, ushanielewa ndio maana nimetofautiana nae kwa kitu hicho, na hawezi kuwa mwanaharakati kwasababu nimeshawahi kukaa nae na kumwambia tufanye harakati hizi kuokoa mziki akasema harakati hizi ni ngumu, kwamba ni nzito siziwezi wakati nyimbo zake zinapigwa, lakini leo namshangaa anavyolia wakati nyimbo zake hazipigwi, watu kama kina Nikki na wasanii wengine ni kama kunguru wasio na mabawa............"

"hawa wasanii wa hiphop hata kwenye tua za basi wanakua hawaongei na wasanii wabana pua, wakiwekwa kwenye hoteli wanasema hawa wabanapua sikai nao, silali nao chumba kimoja, huo ni ushetani na ni upumbavu ambao umekithiri.....wanahiphop wa Tanzania ni wanafki, na ni wachawi wakubwa...hiphop lazima ujue maisha yako...wamekuwa ni wanafki wa kuongea kwenye radio...." zaidi msikize hapa chini

ISHU YA MKATABA WA RICK ROSS NA REEBOK KUKATISHWA TAARIFA NI KWAMBA BADO INAENDELEA

.
.
Wakati kundi la kutetea Wanawake la Ultra Violet likisherehekea uamuzi wa kampuni ya Reebok kusitisha mkataba wake na rapper Rick Ross kutokana na mashairi yake kuonekana yakisifia ubakaji, baadhi ya watu walio kwenye timu ya Rick Ross wameonekana kukerwa na uamuzi wa kampuni ya Reebok.
Japo Rick Ross mwenyewe hajaongea chochote mpaka sasa, rapper Meek Mill ambae yuko chini ya Maybach Music ya Rozay amelianzisha baada ya kuidiss Reebok kwa kusema lebo ya viatu vyao ni sawa na FILA, yani lebo ya kizamani.
.
Hawa ni sehemu ya waliojitokeza kupinga mashairi ya Rick Ross ndio maana waliandamana na kuitaka kampuni hiyo impige chini Rozay kama inataka biashara iendelee

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz