Lupita:Mwanamke mrembo zaidi 2014



Lupita alishinda tuzo ya Oscar kwa kipawa chake cha kuigiza katika filamu 12 Years a Slave

Jarida la People limemtangaza Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.

Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu '12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki hii ya jarida hilo.


Katika orodha yake ya wanawake 50 warembo duniani,Lupita amewapiku waigizaji maarufu akiwemo Kerry Washington, ambaye pia alishiriki katika filamu hiyo na mwanamuziki Pink ambao walikuwa katika nafasi ya 10 na 5 mtawalia.



Jarida la People limemtaja Lupita kuwa mwanamke mrembo

Stacy Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.

Hatua ya Jarida la People ambalo huchapishwa kila wiki nchini Marekani na kusomwa na karibu watu milioni 40, kumkubali Lupita kama mwanamke mrembo duniani, ni kama tuzo kivyake kwa muigizaji huyo ambaye amegonga vichwa vya habari nchini Marekani tangu kushinda

Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.

"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufiia chochote maishani mwao.
Taarifa zinazohusiana

0 comments:

Mbinu za CIA kubadilishwa Marekani


Stakabdhi za CIA Kufichuliwa kwa umma
Bunge kufichua siri za CIA
Kamati ya bunge la Marekani kuhusu ujasusi imeidhinisha kuwekwa wazi kwa sehemu mojawepo ya ripoti iliyoiita ya "ukatili" ilioelezea jinsi maafisa wa shiriki la upelelezi la Marekani CIA linavyowahoji wanatuhumiwa wa ugaidi.
Lakini wanakamati wanasema kuwa itachukua muda kabla ya uchunguzi huo kuwekwa wazi kwa umma.
Sehemu ya ripoti iliyofichuliwa inasema kuwa idara ya CIA kila mara ilipotosha serikali kuhusiana na mtindo wake wa kuhoji washukiwa wa ugaidi wakati wa utawala wa Rais George W Bush.
CIA inapinga baadhi ya matokeo ya taarifa hiyo huku ikikiri kutenda matendo ambayo hayakuafikiana na sera za Marekani.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya baraza la Senate Dianne Feinstein anasema matokeo ya kura iliyopigwa kuhusu ripoti hiyo inaonesha wabunge 11-3 waliipigia mswada huo kura huku akisema ni uchunguzi wa matokeo yanayotamausha.
 
Stakabdhi za CIA Kufichuliwa kwa umma
"ripoti hiyo inaonyesha dhuluma inayoenda kinyume na hadhi ya taifa letu,''alisema Dianne
Hii inatia doa historia ya taifa letu na ambayo hairuhusiwi kamwe kufanyika. ''Hivi sivyo wamarekani wanavyofaa kufanya." Mwanasiasa huyo wa chama cha Democrat kutoka Carlifonia amesema.
Taarifa ya wanahabari inasema kuwa japo baadhi ya wanakamati wa chama cha Republican walikashifu ripoti hiyo kwa pamoja na wa Democrats, kulionyesha waziwazi mgawanyiko uliopo ndani ya wajumbe hao.
Matokeo ya uchunguzi huo uliyomo katika kijitabu cha ukurasa 500, yatatumwa kwa Rais Barack Obama ili kuchunguzwa, kutiwa saini, kisha kutolewa kwa umma.

0 comments:

DODOMA MKO TAYARI?? UZINDUZI WA MABASI YA SHABIBY PALE LOYAL VILLAGE UTAAMBATANA NA BURUDANI KIBAO KIINGILIO NI BUREE!! UNAJUA NIN BAS....RECHO THT ATAHUSIKA SANA,,,,,SOMA ZAID HAPA




Leo tar 4/4/2014 ndio ile siku ya party ya uzinduzi wa basi mpyaaaa 10 za Shabiby bus.Inafanyika Royal village,Wasanii kibao kama vile Recho na wengine kibao KAMA onee 6 na mchungaji zayumba....unajua nene hii si ya kukosa coz wasanii hao hot watausika,Hakuna kiingilio

0 comments:

PICHA TATA ZA JOKATE AKIWA NA GODZILLA NI SHIDA HEMBU TAZAMA JOKETI ALIVYOKAMATIWA KIUNO



0 comments:

Hiki ndicho kitakachofanyika kwenye Club za New Maisha Morogoro,Mbeya,Dar na Mtwara Weekend hii.

Club Maisha (4)New Maisha Club ndiyo Club pekee Tanzania iliyofanikiwa kuwa na matawi mengi mikoani ukitoa Dar es salaam ambayo ndiko ilikoanza,kwa sasa New Maisha Club ipo Morogoro,Mtwara,Dodoma na Mbeya ambapo kuna baaadhi ya party hufanyika siku moja kupitia club zote hizi.
IMG-20140403-WA0015(1)New Maisha Club 87.8 Mbeya Jumapili ya April 06 Kutakua na usiku wa vyuo ambao utasindikizwa na Roma Mkatoliki huko Roma ataenda pia kuzindua wimbo wake mpya wa K.K.K
IMG-20140403-WA0017New Maisha Club 88.5 Morogoro Jumapili April 06 kutakua na Shilole utakua ni uzinduzi wa video ya Chuna Buzi ambapo kwa Shilole atasindikizwa na Nuh Mziwanda na Darasa.
IMG-20140331-WA0018New Maisha Club 88.4 Mtwara April 06 kutakuwa na Mirror kwenye Mirro’s Night upande wake atakua na Jordan da Prince.
IMG-20140403-WA0018New Maisha Club Dar es salaam 88.5 kutakua na uzinduzi wa wimbo wa Agaba wa Suma Mnazaleth ambaye atasindikizwa na Stamina,Cyril,Tash&Juru,Mabeste,Water Chilambo,Darasa,Messen&Defatality Team.

0 comments:

PROF. JAY – LINI SERIKALI MTASIKIA KILIO CHA WASANII

Msanii mkongwe katika game la Bongo Flava Joseph Haule aka Prof. Jay aliyewahi ku-hit na ngoma kibao kama Bongo Dar es salaam, Ndiyo Mzee, Kamili Gado nk. Kwa sasa

Jay kamwaga lawama za wasanii kuibiwa kazi zao baada ya yeye mwenyewe kujionea udhaifu unao sababisha taizo hilo, kwa machungu kaamua kuweka wazi leo tatizo hilo ililiweze kupatiwa ufumbuzi kwa.

“Tatizo kubwa na la miaka nenda rudi kwenye sanaa Yetu iwe Muziki, Filamu na sanaa nyingine ni wizi wa wazi wazi wa kazi zetu, Inauma sana unapopita Ubungo Mataa, Mwenge, na sehemu mbali mbali za katikati ya jiji na kukuta ndugu zetu kabisa wakiuza kazi mpya za wasanii mbalimbali ambazo sio orignal na bila ridhaa ya wasanii wenyewe,.” Prof. Jay alizidi kusema “Mbaya zaidi ni pale tunapowakamata na kuwapeleka polisi kesho yake unawakuta wameachiwa na wanaendelea na kazi yao na ukiwahoji ni nani anayetengeneza hizo CD na DVD hawataji kamwe.” Pia kuna wale ambao wana vibanda vyao vingi nao pia utakuta bila aibu wameweka matangazo..Tuna burn nyimbo mpya za Bongo Flava, Bongo Movies.. CD, DVD, Tunaingiza nyimbo kwa Bluetooth na kwenye flash kwa bei karibu na bure, yani imekuwa kama ni halali kwao wakati hilo ni jasho la msanii na hanufaiki nalo hata kidogo, Je kweli tumeshindwa kulitatua hili tatizo sugu au mpaka wasanii tuchukue sheria mikononi kama madereva wa Boda boda ndio mtakisikia hiki kilio chetu.”

0 comments:

HIVI UNAJUA KWAMBA NANDO WA BIG BROTHER AWA MPAMBE WA WEMA SEPETU

Siku Wema Alipoenda kufanya Timbwili kwenye Ofisi za Magazeti Maarufu Bongo Global Publishers Aliongozana na Baadhi ya Wapambe wake Ambao mmoja wapo alikuwa ni Mshiriki wa Big Brother Africa Aliyeiwakilisha Bongo Mwaka Jana anayejulikana kama Ammy Nando ...Kama anavyoonekana kwenye picha hapo alikuwa anajificha asipigwe picha na waandishi habari nje za ofisi za Global Publishers....Najiuliza na yeye Amefuata mkumbo wa Kina Petit na Martin Kadinda ?

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz