TAZAMA PICHA ZA VURUGU WANAFUNZI WA KENYA WALIPOPIGANA NA POLISI KUPINGA ADA KUONGEZWA

Wanafunzi walitawanywa kwa kutumia gesi ya kutoa machozi
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya wamezua vurugu wakipinga mpango wa serikali kutaka kuongeza karo katika vyuo vikuu vyote vya umma.
Polisi walipambana na wanafunzi hao kwa kutumia gesi ya kutoa machozi kutawanya wanafunzi hao ambao walizua vurugu mjini na kuwapora abiria huku wakiharibu magari ya umma na yale ya abiria katika barabara kuu ya Uhuru katikakati ya jiji la Nairobi.
Pia waliripotiwa kuvunja maduka na kuharibu mali ya watu.
Wachuuzi walilazimika kuondoka mjini huku polisi wakipambana na wanafunzi hao ambao waliungana kutoka vyuo vikuu mbali mbali kote nchini Kenya.
Awali maandamano yao yalikuwa salama ingawa baadaye wanafunzi hao walioanza kuandamana tangu saa nne asubuhi walianza kuzua rabsha na kulazimisha polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya.
Wanafunzi hao wanaandamana kupinga mapendekezo ya serikali kuongeza karo ya vyo vikuu , ingawa waziri wa elimu ya juu Profesa Jacob Kaimenyi amesema kuwa serikali bado haijatoa tamko rasmi ikiwa wanafunzi wa vyuo vikuu watalazimika kuongeza karo.
Alisema kuwa ripoti kuwa karo itaongezwa sio sawa na ni za kupotosha akisisitiza kuwa ikiwa jambo kama hilo litafanyika litahitajika kutangazwa na baraza la vyuo vikuu nchini humo baada ya makubaliano kufikiwa.
Wanafunzi hao wanapinga mpango wa serikali wakisema kuwa kuambatana na mfumuko wa bei, karo yao haipaswi kuongezwa na kwamba serikali inapaswa kushauriana nao kabla ya kufikia hatua zozote za kuongeza karo.
Wanafunzi watano wameripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo

0 comments:

PICHA MAELFU WAMZIKA ADAM KUAMBIANA KINONDONI DAR



Mashada yakiwa tayari juu ya kaburi la marehemu Adam Philip Kuambiana, muda mfupi baada ya shughuli za maziko kukamilika.

Jacob Steven 'JB', akiweka shada kwenye kaburi. 
Msanii wa fialmu Bongo, Mariam akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Kuambiana.
Mwili wa marehemu Kuambiana ukiwasili makuburini tayari kwa shughuli za kuusitiri.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Kuambiana likishushwa kaburini.
Jeneza likishushwa kaburini.
Msanii wa filamu, Richie Richie akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Kuambiana.
Baadhi ya mafundi wakichanganya zege kujengea kaburi.
Mafundi hao wakikamilisha shughuli za kujengea kaburi hilo.
Mchungaji akiweka msalaba kwenye kaburi.

0 comments:

Watu 46 wauawa katika mlipuko Nigeria

 
Watu 38 wauawa katika milipuko miwili mjini Jos Nigeria
Takriban watu 46 wameaga dunia na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko miwili mikubwa kutokea nchini Nigeria katika mji wa Jos.Milipuko hiyo imetokea katika soko lenye shughuli nyingi .
Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa amehesabu miili 40 ikipelekwakatika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja iliyoko JOS.
Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid aliye mjini humo anasema kuwa kuna hofu ya watu wengi kujeruhiwa hasa kwa kuwa soko hilo lilikuwa na idadi kubwa ya watu.
Aidha anaarifu kuwa taharuki ietanda katika eneo hilo baada ya vijana waliopandwa na hasira kufunga mabarabara ya kuingia na kutoka mjini humo na kuzua hofu ya makabiliano.
Mji wa Jos itakumbukwa iliwahi kushuhudia mapigano mabaya zaidi baina ya makundi ya vijana Waislamu na wale Wakristu iliyosababisha maafa mengi.
Mabomu hayo yanasemekana kuwa yalikuwa yametegwa moja katika lori na lingine katika gari la uchukuzi wa abiria na yakalipuka kwa mpigo moja katika soko la lingine karibu na hospitali.
Hakuna aliyekiri kutekeleza mashambulizi hayo ijapokuwa jimbo hilo limewahi kushambuliwa na kundi la Boko Haram zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Watu 38 wauawa katika milipuko miwili mjini Jos Nigeria

Watu 38 wauawa katika milipuko miwili mjini Jos Nigeria
Jimbo la Platue liko mpakani kati ya waislamu wanaoishi Kaskazini mwa Nigeria na Wakrstu ambao wanaishi Kusini .
Jimbo hili limewahi kushudia mapigano baina ya wakulima wakristu wa tabaka la Berom na waislamu wafugaji wa kuhamhama wa tabaka la Fulani.
Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.
Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.

0 comments:

Sumry yatoa ubani wa Sh 5.5M ajali Singida


“Tangu kutokea kwa ajali hiyo kijiji kimeendelea kupata idadi kubwa ya wageni kutoka sehemu mbalimbali kuja kutoa pole kwa wafiwa. Tunatarajia kufanya sala maalumu kwenye eneo la tukio kesho (leo), kuwaombea ndugu zetu.
Kholani alisema pia Mbunge wa Singida Magharibi, Mohamed Missanga ametoa Sh600,000 na wakazi wa Tarafa ya Ihanja waishio jijini Dar es Salaam pia wamechanga Sh600,000.

 Uongozi wa Kampuni ya Mabasi ya Sumry ya Sumbawanga, Rukwa umetoa ubani wa Sh5.5 milioni kwa familia za ndugu na jamaa waliofariki dunia kutokana na ajali ya moja ya mabasi yake iliyotokea Aprili 28 katika Kijiji cha Utaho, Wilaya ya Ikungi, Singida.
Katika ajali hiyo, watu 19 wakiwamo polisi wanne, walifariki papohapo baada ya kugongwa na basi hilo lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori na mwendesha baiskeli ambaye alipoteza maisha katika eneo hilo baada ya kugongwa na lori hilo. Wakazi hao waliogongwa walikuwa wamekusanyika kushuhudia ajali hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hipoliti Daniel Kholani alisema rambirambi hiyo ilikabidhiwa kwa Serikali ya Kijiji na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone ambaye naye alichangia Sh100,000.
Kholani alisema pia Mbunge wa Singida Magharibi, Mohamed Missanga ametoa Sh600,000 na wakazi wa Tarafa ya Ihanja waishio jijini Dar es Salaam pia wamechanga Sh600,000.
“Tangu kutokea kwa ajali hiyo kijiji kimeendelea kupata idadi kubwa ya wageni kutoka sehemu mbalimbali kuja kutoa pole kwa wafiwa. Tunatarajia kufanya sala maalumu kwenye eneo la tukio kesho (leo), kuwaombea ndugu zetu.”
Kholani alisema wakazi wa kijiji hicho, Mussa Mohammed, Suku Abdallah na Ayubu Ramadhani bado wamelazwa hospitalini wakiendelea kutibiwa majeraha waliyoyapata kwenye ajali ya basi hilo ambalo bado lipo Kituo cha Polisi Ikungi.

0 comments:

Mkapa atoa tahadhari kuhusu Katiba Mpya

 

Aeleza umuhimu wa wananchi kuvumiliana katika mjadala hata kama watahitilafiana.

  Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amewataka Watanzania kuwa waangalifu ili mchakato wa Katiba Mpya usiwe sababu ya kupigana au kufarakana ili kupata Katiba itakayoendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na ushirikiano.


Mkapa alitoa wito huo juzi, alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi nyumba 30 za watumishi wa vituo vya huduma ya afya mkoani hapa zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS Foundation kwa zaidi ya Sh1.9 bilioni.


“Vyovyote mchakato wa Katiba utakavyoishia, tuhakikishe tunabaki na amani na utulivu wetu kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu, tuhitilafiane bila kupigana,” alisema.


Alisema Watanzania wanapaswa kwa pamoja wasiiharibu nchi yao na kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho, vinaendelea kuwaenzi waasisi wa Taifa kwa uadilifu mkubwa.


Akabidhi nyumba


Akikabidhi nyumba hizo, Mkapa alisema ana imani wananchi wanaohudumiwa na zahanati 15 zilizojengewa nyumba hizo wataendelea kufaidika na huduma bora kwa kuwa watumishi wameboreshewa mazingira ya kazi.


“Kama mnavyoona nyumba hizi ni za kisasa, zina maeneo muhimu yote yanayokidhi mahitaji ya binadamu, zipo imara na zimekidhi viwango vya ujenzi vinavyostahili,” alisema.


Aliitaka halmashauri zinazohusika kuhakikisha nyumba hizo zinatumika kama ilivyokusudiwa, kutunzwa vizuri na kutengewa bajeti ya kutosha kwa ajili ya ukarabati pale utakapohitajika ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.


Vijiji vilivyonufaika vipo katika wilaya za Singida Vijijini, Iramba na Manyoni.

0 comments:

Nguruwe kupigwa risasi India




MAKALA YA AFYA:Wanaharakati wamepinga vikali kuwaua Nguruwe wakisena ni kinyume na haki za wanyama 

0 comments:

Hamad Rashid: Nitagombea urais 2015


 


Asema atachagua chama chochote na ataamua baadaye awanie upande gani

  Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed amesema anapanga kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais katika Uchaguzi Mkuu mwakani.


Akizungumza katika mahojiano maalumu hivi karibuni mjini Dodoma, Hamad Rashid alisema: “Kama Mwenyezi Mungu akinijalia uhai na uzima mwakani, ninatarajia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais ama wa Muungano au wa Zanzibar.


“Ila sijaamua kama ni Bara au Zanzibar; kama ni chama cha CUF au kingine, hayo yote yatakuja baadaye,” alisema Hamad Rashid.


Mohamed ambaye ana mgogoro mahakamani na chama chake cha CUF, ametoa kauli hiyo wakati tayari viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), CUF kikiwamo wanajipanga kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi ujao.


Mbali na CUF, vyama vingine vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi na Chadema ambavyo pia vinakusudia kusimamisha mgombea mmoja kwa nafasi za ubunge na udiwani, lengo likiwa kukabiliana na nguvu ya chama tawala, CCM.


Hamad Rashid aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu CUF, alifutwa uanachama Januari 4, 2012 na Baraza la Uongozi la chama hicho kwa madai ya kukihujumu kwa mujibu wa kifungu 63 (1) (j) na 64 (1-5) cha Katiba ya CUF. Wengine waliotimuliwa pamoja na Hamad ni Doyo Hassan Doyo, Shoka Hamis Juma na Juma Said Sanani.


Sakata la Hamad kuvuliwa uanachama lilianza baada ya kutangaza kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho katika uchaguzi wa mwaka huu, nafasi inayoshikiliwa na Seif Shariff Hamad ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar.


Hata hivyo, Januari 10, 2012 Hamad Rashid na wenzake waliiomba Mahakama iwatie hatiani wadhamini wa CUF, kwa kukiuka amri ya Mahakama kutokana na uamuzi wa Baraza la Taifa la Uongozi la chama hicho kuwafukuza uanachama wakiwa tayari wameweka zuio.


Baadaye Septemba mwaka jana, Hamad alikaririwa na gazeti moja akisema suluhu yake na CUF haiwezi kupatikana kwa kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo hakubaliani nayo ndani ya chama hicho.

0 comments:

Mlipuko:19 waripotiwa kupoteza maisha Nigeria





Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini sitaka kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.

Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.

Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waliojeruhiwa walikimbizwa hosipitalini


Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa. Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja

Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Lakini shambulizi la bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao.

0 comments:

UNAAMBIWA JOHARI AMWAGA MACHOZI LIVE NI BAADA YA RAY NA CHUCHU KUZIDISHA MAPENZI MOTO MOTO MPK JOTO LINAONA WIVU:



Hot news is that staa ray the great leo kupitia mitandao ya jamii alizungumza kuwa anampenda sana chuchu hans, na hakuna atakayeweza kuwatenganisha, na kwa kuliaprove hilo ndipo alipoamua kuweka picha hii yapo juu ikiwa ni ishara ya mahaba na upendo kwao.

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz