TASWIRA MBALIMBALI ZA MAJERUHI KATIKA VURUGU ZA WAISLAMU NA WAKRISTU MKOANI GEITA

Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Yasin Rajabu na hapa akiwa amelazwa katika wod namba 8 Hospitali ya wilaya ya Geita kwaajili ya kupatiwa matibabu.
Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Said Ntahompagaze aliyejeruiwa mguu wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.
Hivi ndivyo unavyoonekana mguu wa Said Ntahompagaze aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.
Majeruhi Vicent Damon akiwa amelazwa wod na 8 hospitali ya wilaya ya Geita aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.
Majeruh Sadick Yahaya.
Majeruhi Ramadan aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha fukuto kubwa la vurugu zilizosababisha shughuli mbalimbali kusimama.

Machafuko makubwa yametokea leo katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini  wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.
Habari za kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wadini ya kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo.
Imeelezwa kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya waislamu.
Tukio hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama kuwasili katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la kuifunga.
Wakati wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lililpambwa kwa maandishi BWANA YESU ASIFIWE, YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.
Kutokana na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao walitumia mapanga na majambia.
Hata hivyo wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.
Mbali na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na Said Ntahompagaze(45), Sadick Yahaya(40), Yasin Rajab(56), Vicent Damon(22), wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika hospital ya wilaya ya Geita.
Hata hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.
Jeshi la polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa 4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.
Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya kidini.PICHA NA HABARI global publishers

0 comments:

TANZANIA YASHINDA VIVUTIO VITATU MAAJABU SABA YA ASILI AFRIKA, NI MLIMA KILIMANJARO, NGORONGORO CRATES NA MBUGA YA SERENGETI



Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka…
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kamavinavyoonekana.
Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Utalii TTB.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika MasharikiKatika picha kulia ni Waziri waMaliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wawakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzaniaakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia.
Mbunge Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teyrol walipokutana katika hafla hiyo.
Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa wengine wa bodi hiyo wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw. Miskanji.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Mkurugenzi wa Hifadhi za taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge waliohudhuria katika hafla hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na kushoto ni David Kafulila.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki wakati alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa ajili ya utoaji tuzo hizo.
Mama Tunu Pinda wa pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka Seven Natural Wonders.
Mabalozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw. Godbless Lema  kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB)  Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.
Bw Allan Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi  katika hafla hiyo, kushoto ni Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.
Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
 Balozi wa Kenya nchini Tanzania akizungumza na Balozi Charles Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB na Mkurugenzi wa bodi hiyo Dk. Aloyce Nzuki wakati wa hafla hiyo.picha;habari na global publisher

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz