UCHAFU WA MAZINGIRA WAKITHIRI SOKO KWA MOROMBO JIJINI ARUSHA.
Wananchi mkoani Arusha wametakiwa kuwa na uhuru wa kuteuwa
na kawatumbua watu wanatakiwa kufanya doria ya ulinzi shirikishi katika mitaa
yao nyakati za usiku.
Akuzungumza na waandishi wa habari msaidizi wa mkuu wa
kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha Ndg.Yona Maziba amesema kuwa ili
kuepukan na makundi ya watu wanaoigiza kuwa ni polisi jamii na kumbe ni vibaka
wanaotumia fursa hiyo kuwateka wakazi wa mtaa husika na kuwachukulia vitu vyao
pindi wanapo nyumbani nyakati za usiku.
Amesema pamoja na kutoa semina kwa makamanda waandamizi wa
ulinzi shirikishi lakini bado wanakabiliwa na makundi yasiyo sahihi na teule
kwa kufanya shughuli hiyo na ndiyo maana hali hiyo inawawia vigumu wao wenye
kutambua ni makundi ya aina gani yanajishughulisha na utekaji na kuigiza wao
kama polisi jamii.
Pia ameongeza kuwa kila mwananchi anatakiwa kuwa na uhuru wa
kuhoji makundi ya namna hiyo kuwa kama wana vitambulisho vyenye kuonyeasha wao
ni akina nani kwani huwa kuna mavazi maalumu wanayovaa kwaajili ya lindo.
Kamanda Yona ameongeza kuwa uzalendo ni fursa yetu binafsi
hivyo katika hilo inahitajika wananchi kuwa wazalendo kwani unapo kuwa mzalendo
na nchi pia hata na mtaa wakon ni dhahiri kuwa utajilinda na kuulinda mtaa wako
na nchi yako kwa ujumla kwa kufichua watu wanaojihusisha na tabia hizo za
utekaji na uporaji wa mali za watu ili waweze kufikishwa mahali husika na
kupewa adhabu stahiki.
0 comments: