TAMATI YA BONANZA A.J.T.C. KUJULIKANA LEO



Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wanatarajiwa kumaliza bonanza liloanza siku ya jumatano chuoni hapo 
Akizungumza na BLog hii kwa nyakati tofauti mwalimu wa michezo chuoni hapo amesema kuwa mashindano yaliyoandaliwa na kamati ya michezo yana malizika leo.
Baadhi ya michezo iliyokuwamo ni mpira wa miguu,netball,kucheza karata,kula,kuzunguka viti,kucheza draft na mingine mingi.Alisema lengo ni kutafuta timu bora ya chuo pamoja na kuwafanya wanafunzi kuwa vizuri kiafya na kiakili kwani michezo hujenga mwili kwa kufanya mazoezi.
Pia waalimu wa chuo hicho walihusishwa kwenye mashindano hayo kwa kupewa dhamana ya kuwa marefa kwenye mpira wa miguu pamoja na netball.
Wanafunzi wa chuo hicho walionyesha ushirikiano mzuri kwa kuwashabikia wenzao walipokuwa wakicheza.
Zawadi za washindi wote kwa ujumla zitatolewa leo chuoni hapo baada ya kumalzika kwa michezo yote...

0 comments:

SOMA HAPA WABUNGE WA CCM JUZI WALIVYORUSHIANA MANENO MAZITO KUHUSIANA NA KUUZWA KWA UDA



MBUNGE wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya (CCM), ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa zamani, jana alijikuta katika wakati mgumu wa kuumbuliwa na mbunge mwenzake wa Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), wakati wawili hao wakibishania uuzwaji tata wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA).Hatua hiyo ilijitokeza wakati Mtemvu akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa mwaka wa fedha 2014/2015, na kuungana na wabunge wenzake kadhaa waliotangulia kuchangia, akidai UDA imeuzwa kifisadi bila wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam kushirikishwa.
 Wakati Mtemvu akiendelea kujenga hoja yake, Prof. Kapuya aliomba kumpa taarifa, akimweleza kuwa mbunge kujishughulisha na uwekezaji si dhambi na kwamba UDA imeuzwa kihalali wala hakuna ufisadi kama inavyodaiwa, isipokuwa mbunge huyo anatumika kuwashawishi wabunge kupinga suala hilo. Baada ya Prof. Kapuya kuketi,

0 comments:

Mtawa anyakua ushindi wa uimbaji -Italia



Mtawa wa Italia anyakua ushindi
Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo.
Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki shindano la The Voice.
Scuccia aliyeonekana amevalia mavazi yake ya utawa na msalaba shingoni, alijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa kumfikisha katika ushindi huo.
Mtindo wake wa wimbo wa Alicia Keys, kwa jina 'No One', umetizamwa zaidi ya mara milioni 50 katika mtandao wa You Tube tangu auimbe.
Mtawa huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema kuwa aliamua kushiriki mashindano hayo kufuata ushauri wa Papa mtakatifu Francis, kuwa kanisa liwakaribie zaidi watu wa kawaida.

0 comments:

Ni uhalifu kuwanyanyasa wanawake - Misri

wanawake wa Misri
Kwa mara ya kwanza Misri imepitisha sheria inayotaja unyanyasaji wa wanawake kuwa uhalifu.
Chini ya sheria hiyo wanaume watafungwa miaka 5 gerezani kwa kuwanyanyasa wanawake hadharani au faraghani.
Sheria hiyo imepitishwa kama hatua ya mwisho kuchukuliwa na rais anayeondoka wa Misri Adly Mansour.
'Unyanyasaji umezidi'
Watetesi wa haki za wanawake nchini Misri wamesema kuwa unyanyasaji wa wanawake umefikia viwango vya kuhuzunisha. Utafiti uliofanywa umeonesha kuwa karibu wanawake wote wa Misri wamewahi kupitia unyanyasaji wa aina fulani iwe ya matusi au hata ubakaji.
Utafiti huo umeonesha kuwa hata mavazi ya kufunika mwili wote yanayopendekezwa na sheria za kiislamu nchini humo, hazijawazuia wanaume hao kuwanyanyasa wanawake.
Na sasa inahofiwa kuwa mapinduzi waliofanya mwaka wa 2011 hayakuleta mabadiliko yoyote.
Wanawake wengi wamelalamika kuwa walinyanyaswa wakiwa katika maandamano katika midani ya Tahrir.
'Tatizo liko kwa itikadi mbovu'
Watetesi hao wa haki wanasema kuwa polisi mara nyingi wanawalaumu waathiriwa kuliko wale wanaofanya uhalifu huo.
Sasa sheria hii inachukuliwa kama hatua kubwa sana kusaidia tatizo hilo, ila hofu ni kwa utekelezaji wake. Wadadisi wanasema kuwa itakuwa vigumu zaidi kubadilisha itikadi za watu juu ya unyanuasaji wa wanawake nchini humo .

0 comments:

G7 wakutana Brussels bila Urusi

mkutano wa G7
Viongozi wa mataifa tajiri ya magharibi wanaokutana mjini Brussels wamesema kuwa wako tayari kuweka vikwazo zaidi kwa Urusi iwapo itaendelea kuvuruga amani mashariki mwa Ukrain.
Taarifa ya pamoja ya mataifa ya G7 imesema kuwa Mambo yanayofanywa na Urusi nchini Ukrain hayawezi kubalika kamwe na lazima yakomeshwe.
Huu ndio mkutano wa kwanza wa viongozi hao tangu waifukuze Urusi kama mwanachama.
Urusi ilibumburushwa kutoka G7 kwa kosa lake kubwa zaidi, kuinyakua Crimea kutoka Ukrain.
Viongozi wa mataifa hayo ya G7 wanakutana sasa kwa mara ya kwanza tangu wakati huo.
Ukrain vita vimechacha
Lakini huku wakikutana mapigano yamechacha kati ya serikali ya Ukrain na majeshi yanayo unga mkono Urusi mashariki mwa Ukrain.
Urusi imeendelea kukana kuhusika na mapigano hayo. Miongoni mwa mikutano iliyopangwa Alhamisi hii, waziri mkuu wa Uingereza Davin Cameron atakutana na rais Obama mjini Brussels, ambapo kwa upana zaidi watazungumzia Urusi. Kisha baada ya mkutano huo, David Cameron ataelekea Paris Ufaransa kwa mkutano wa faragha na rais wa Urusi Vladmir Putin.
Katika wiki hii mataifa ya Uropa yamekuwa yakiadhimisha siku ya kuikomboa bara Uropa kutoka utawala wa ki Nazzi katika vita vya pili vya dunia miaka 70 iliyopita.
Huku hayo yakitokea, juhudi za kidiplomasia zimeshika kasi miongoni mwa mataifa ya magharibi kumaliza uhasama kati yao na Urusi.
G7 wamepongeza uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Ukrain na wameirai Urusi kumpokea na kushirikiana na rais mpya wa Ukrain Petro Poroshenko. Pia wameonya kuwa hawatasita kuiwekea Urusi vikwazo zaidi iwapo itakataa kusaidia kurejesha uthabiti Ukrain.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa miaka 17 ambapo G7 inakutana bila Urusi.

0 comments:

NAIBU MEYA AMPANDA KIZIMBANI


NAIBU Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe na Diwani wa Kata ya Levelos, Ephata Nanyaro, wote kutoka CHADEMA, wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kumshambulia mgambo wa jiji, William Mollel.
Mwanasheria wa Serikali, Mary Lucas, aliwasomea shitaka hilo la jinai namba 413/2014  jana mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Patricia Kisinda.
Alisema kuwa Aprili 16 mwaka huu, wakiwa maeneo ya Levelos, madiwani hao wanadaiwa kumpiga, Mollel kifuani na sehemu mbalimbali za mwili, hivyo kumsababishia maumivu mwilini.
Lucas alisema kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo akaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo, huku akiweka wazi kuwa upande wa serikali hauna pingamizi ya dhamana kwa washitakiwa hao.
Madiwani hao walikana shitaka hilo na wako nje kwa dhamana hadi upelelezi utakapokamilika ambapo shauri hilo litarudi mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa Julai 8, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, wananchi kadhaa walionekana wakiwa na barua kwa ajili ya kuwadhamini madiwani hao ambao juzi walitangaza kuwa hawako tayari kudhaminiwa ili waende mahabusu kwenye gereza la Kisongo.

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz