HIZI NDIO TOFAUTI KATI YA MADEMU WA UDSM NA MADEMU WA UDOM :SOMA HAPA UJUE CHUO GANI WANAFUNIKA:
Kuna
tofauti kubwa kati ya mabinti wa UDSM na wale wa UDOM. Mbali na kwamba
wote ni wazuri na wamemeenda vidato lakini zipo tofauti kubwa baina yao
zinazowatofautisha. Kwa ujumla tofauti zao ni hivi zifuatazo;
Muonekano (image)
Binti
wa UDSM mara nyingi atapenda avae vitu mpaka aonekane kama
mwanamitindo. Atajiwekea make up za kila aiana japokuwa tayari ana uzuri
natural. Atataka avae fasheni mpya mpya zinazotokana kwa kuwa yuko town
na mara nyingi hata kama boom haliruhusu kuna wananchi wengi wa
kuwapiga mizinga. Nguo zao wananunulia Mlimani City, Quality Center,
Makumbusho, Mwenge kwa White na maeneo mengine kama hayo. Jinsi
wanavyovyaa unaweza ukawaogopa kudhani ni expensive saaaaana.
Binti
wa UDOM kwa upande mwingine anavaa kawaida tu. Viatu vyake vya
mchomekeo wanavinunua pale SabaSaba lakini waulize wavulana UDOM sasa,
watakwambia binti katoka bomba yule si mchezo. Viatu vyao ni bei za
kawaida na huvumilia hali zote za hewa. Huwa shopping zao wanafanya Saba
Saba.
Sehemu ya kuangalia movie (cinema)
UDSM
huwezi kumpeleka binti kucheka movie room kwako! Sijui eti Hall 3 au
ghetto Survey! Utampeleka Suncrest Quality Center au Mlimani City na
hapo uweke bajeti ya PopCon na mazagazaga kibao ya kucheki cinema.
Binti
wa UDOM wewe tu na laptop yako unamkaribisha chumbani Block 9, 10, etc
maeneo ya Haiti mnacheki movie huku mkinywa maji ya kudownload, bites za
Discount shop au chai. Umemaliza.
Sehemu ya kukutania (Date location)
Kama
unadhani binti wa UDSM utampeleke room yako namba 2409 kule Hall 3
sahau! Kama huna ghetto la ukweli Survey au Sinza au Ubungo Maziwa au
unamiliki nyumba kabisa jua imekula kwako. Sehemu ya kukutania lazima
iwe ya kueleweka na treatment isomeke vizuri kama misosi iliyosimama,
Pizza, Burger, Chicken Chips, etc. Hapo lazima Bamaga upajue vizuri,
Mikocheni na Sinza. Kishushio Savanna au Red Bull. Mjomba huna hivyo
UDSM utawapata wa kuhesabu kukusikiliza maelezo yako ya kuunga unga.
Binti
wa UDOM yeye hata hajali. Wewe tu, uwe kule porini mnapaita Ng’ox au
Social Room kwako atakuja. Mtengenezee chai kwa ule mkate wako wa juzi
halafu anza kumwaga point zako. Huna haja ya kupajua Area D, Area C wala
Lodge za Area A ila ukikosea ukakuta mwenye kaupepo ka jiji lazima kuku
wa Club Maisha na 84 ujue bei yake.
Upatikanaji wao (Availability)
Binti
wa UDSM atakuona akitaka kukuona si kinyume chake. Ukimpigia simu
mkutane atakupa sababu kibao utabaki kichwa kinakuuma ila yeye
akikupigia simu mkutane hataki kusikia sababu yako hata moja. Anapenda
yeye awe na control.
Binti
wa UDOM yeye anaelewa principle ya give and take vizuri sana. Anaelewa
mla lazima aliwe na anaelewa ili uhusiano uwepo lazima kila mtu aplay
part yake. Ukimpigia simu baada ya dakika au saa chache utamuona na
wanapenda kutembea na wavulana wao campus. Kama unabisha angalia idadi
ya mabinti wa UDSM wanaotembea na boys ndani ya campus na wale wa UDOM
wanaofanya hivyo ndani ya campus.
Mtazamo wao kuhusu mapenzi (Perception of love)
Binti wa UDSM atakupenda kwa ile ulichona nacho. Kichwa class, una hela au famous. Nje ya hapo ni wa kuhesabu bro.
Binti
wa UDOM atakupenda jinsi ulivyo hasa kama shule kasoma Songea huko kwao
vijijini chuo katua Dodoma, ila ukikuta ana kahewa ka Dar kidogo lazima
utasanda. Yale yale.
Mwandishi wa Makala hii amejitambulisha kuwa ni mhitimu wa Digrii ya Ukandarasi na sasa ni chizi hospitali ya Lutindi Tanga.
SOURCE: ORIGINAL K
0 comments: