PROF. JAY – LINI SERIKALI MTASIKIA KILIO CHA WASANII

Msanii mkongwe katika game la Bongo Flava Joseph Haule aka Prof. Jay aliyewahi ku-hit na ngoma kibao kama Bongo Dar es salaam, Ndiyo Mzee, Kamili Gado nk. Kwa sasa

Jay kamwaga lawama za wasanii kuibiwa kazi zao baada ya yeye mwenyewe kujionea udhaifu unao sababisha taizo hilo, kwa machungu kaamua kuweka wazi leo tatizo hilo ililiweze kupatiwa ufumbuzi kwa.

“Tatizo kubwa na la miaka nenda rudi kwenye sanaa Yetu iwe Muziki, Filamu na sanaa nyingine ni wizi wa wazi wazi wa kazi zetu, Inauma sana unapopita Ubungo Mataa, Mwenge, na sehemu mbali mbali za katikati ya jiji na kukuta ndugu zetu kabisa wakiuza kazi mpya za wasanii mbalimbali ambazo sio orignal na bila ridhaa ya wasanii wenyewe,.” Prof. Jay alizidi kusema “Mbaya zaidi ni pale tunapowakamata na kuwapeleka polisi kesho yake unawakuta wameachiwa na wanaendelea na kazi yao na ukiwahoji ni nani anayetengeneza hizo CD na DVD hawataji kamwe.” Pia kuna wale ambao wana vibanda vyao vingi nao pia utakuta bila aibu wameweka matangazo..Tuna burn nyimbo mpya za Bongo Flava, Bongo Movies.. CD, DVD, Tunaingiza nyimbo kwa Bluetooth na kwenye flash kwa bei karibu na bure, yani imekuwa kama ni halali kwao wakati hilo ni jasho la msanii na hanufaiki nalo hata kidogo, Je kweli tumeshindwa kulitatua hili tatizo sugu au mpaka wasanii tuchukue sheria mikononi kama madereva wa Boda boda ndio mtakisikia hiki kilio chetu.”

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz