ANGALIA SHOW YA JAYDEE ILIVYOFURIKA WATU NDANI YA NYUMBANI LOUNGE..!!
Hivi
ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga
jijini Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada
mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye
anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii
wanamuziki mbali mbali watapanda jukwaani aliwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la
Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
Wadau
mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu hivi sasa
kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa
muziki.
Ndani
ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku
wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama
ilimradi tumsapoti Dada yetu.
Getini mambo yako namna hii.
Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.
Burudani ya Utangulizi ikiendelea
0 comments: