KASHFA WIZARA YA AFYA: Yaajiri zaidi ya 'Madaktari' 80 wasiokuwa na sifa
Wiki moja iliyopita wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa orodha
ya majina na vituo vya kazi kwa waajiriwa wapya wa kada ya Afya kwa
mwaka 2012/13 wakiwemo madaktari(Medical Doctors) 260. Zaidi ya
wadaktari 500 wenye sifa stahiki walioomba ajira hizo wakiachwa kwa
kukosa nafasi.
Lakini cha kuchangaza katika orodha hiyo hiyo kumegundulika zaidi ya
majina 80 ya watu waliochaguliwa kwenda kufanya kazi za
kidaktari(Medical Doctor) wakiwa hawana sifa kabisa yaani hawakuwahi
'kitaaluma' kufuzu kuwa madaktari wa kuweza kutibu watu hapa Tanzania.
Sifa kuu zilizokuwa zinahitajika ili kuweza kuajiriwa, mbali na sifa za
msingi za kawaida(Uraia wa Tanzania, usiwe umestaafu nk) ni:
1/Shahada ya kwanza ya Utabibu(1st Degree of Doctor of Medicine)
2/Cheti cha kumaliza mafunzo kwa vitendo na kufaulu(Internship certificate)
3/Leseni 'hai' ya kufanyakazi za Kitabibu nchini Tanzania(Medical Practice Lecence(Active) From Medical Council of Tanganyika).
Hatua hii tayari imezaa kelele na manung'uniko mengi kutoka kwa baadhi
ya madaktari waliokosa nafasi hizo za ajira na wakati huo huo imezaa
woga kwa wagonjwa kuhusu ni kwa vipi watahudumiwa na madaktari hao
'vihiyo'.
SOURCE: Ofisi ya Msajiri wa Madaktari(Medical Council of Tanganyika
0 comments: