Wayne Rooney afanyiwa muendelezo wa tiba wa kukuza nywele.

Wayne-Rooney-twitter-1949401  Mshambuliaji tegemeo wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United Wayne Rooney hivi majuzi alifanyiwa “tiba” ya kukuza nywele zake ikiwa ni muendelezo wa tiba ya kwanza aliyopewa miaka miwili iliyopita ya kutibu “upara” ambao ulikuwa unamnyemelea kwenye kichwa chake. Rooney alifanyiwa tiba hiyo maalum ambapo nywele zilizoko kisogni kwake zilitolewa na kupandikizwa kwenye utosi ili kuondokana na upara uliokuwa unaongezeka siku hadi siku . Rooney alifanyiwa ‘upandikizaji” huo wa nywele zake mwenyewe kwenye hospitali maalum ya tiba za nywele huko London iitwayo Harley Street Hair Clinic na imemgharimu paundi 15,000 ambazo ni zaidi ya milioni 20 kwa fedha za Kitanzania .
Rooney alitoka rasmi baada ya tiba hiyo ya pili kwenye tamasha la mwanadada Rihanna lililofanyika kwenye ukumbi wa Manchester Arena  ambapo alikuwa na mkewe wakisherehekea mwaka wa tano wa ndoa yao .
Rooney ambaye hivi karibuni alimkaribisha duniani mtoto wake wa pili wa kiume amekuwa kwenye hali ya sintofahamu juu ya mustakabali wake wa muda mrefu na klabu ya Manchester United ambapo tetesi kadhaa zimemhusisha na kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya kukerwa kwa kuchezeshwa kwenye nafasi tofauti na nafasi ya ushambuliaji anayoipenda zaidi.                                                                                              Wayne-Rooney-twitter-1949401

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz