KAMANDA MPINGA AFUNGA MAFUNZO YA MADEREVA 278 WA PIKIPIKI ZA MIGUU MIWILI (BODABODA) GONGOLAMBOTO JIJINI DAR
KAMANDA MPINGA AFUNGA MAFUNZO YA MADEREVA 278 WA PIKIPIKI ZA MIGUU MIWILI (BODABODA) GONGOLAMBOTO JIJINI DAR
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga akiongea na
kuwaasa madereva wa Bodaboda wakati wa kufunga mafunzo hayo. Kushoto
kwa Kamanda ni Rais wa AAT Mr Nizan Jivan, CEO wa AAT Mr Yusuf Aghor na
Mweka hazina wa AAT Mr Pepe.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP Mohammed Mpinga akikabidhi cheti kwa mhitimu Mwanamke aliyehitimu mafunzo
ya Elimu ya Usalama Barabarani yaliyotolewa kwa madereva wa Bodaboda
Dsm na Kikosi cha Usalama Barbarani kwa kushirikiana na AAT (Automobile
Association of Tanzania) kwa ufadhili wa chama cha mashindano ya Magari
Duniani (FIA) wakati ufugaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika Gongolamboto
10/07/2013. Anayeangalia ni Rais wa AAT Mr Nizan Jivan
Mr
Nizan Jivan Rais wa Automobile Association of Tanzania (AAT) akiongea
na madereva wa Bodaboda wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika
Gongolamboto – Dar es salaam 10/07/2013. Kulia ni Mr Yusuf Aghor CEO wa
AAT na kushoto ni ASP Swai wa Makao Makuu ya Traffic Dsm.
Mr
Nizan Jivan Rais wa Automobile Association of Tanzania (AAT) akipokea
zawadi maalum kutoka kwa wahitimu wa Mafunzo ya dereva wa BODABODA
mkoani Dar es Salaam kama shukrani yao ya pekee kwa kudhamini mafunzo
haya bure kwa madereva wa Bodaboda, ufugaji wa mafunzo ya elimu ya
Usalama Barabarani kwa madereva wa Bodaboda ulifanyika Gongolamboto Dsm
tarehe 10/07/2013.
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP Mohammed R. Mpinga (kushoto)
akikabidhiwa Tuzo maalum ya ushiriki wake katika kusimamia mafunzo ya
Bodaboda mkoa wa Dar es Salaam. Tuzo hiyo alikabidhiwa na Rais wa
Automobile Association of Tanzania (AAT) Mr Nizani Jivan wakati wa
ufungaji wa mafunzo ya elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa
Bodaboda tarehe 10/07/2013 Gongolamboto – Dar es salaam.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP Mohammed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na Rais
wa Automobile Association of Tanzania (AAT) na wadau mbalimbali
waliohudhuria katika ufugaji wa mafunzo ya elimu ya Usalama Barabarani
kwa madereva wa Bodaboda, tarehe 10/07/2013 Gongolamboto - Dsm.
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP Mohammed R. Mpinga akikabidhi
cheti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Elimu ya Usalama Barabarani
kwa madereva wa Bodaboda katika ufugaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika
tarehe 10/07/2013 Gongolamboto – Dsm.
Madereva
Bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam wakipokea kiapo chao cha utii
kuashiria kuwa mafunzo ya Elimu ya Usalama Barabarani waliyoyapata
darasani sasa watayafanya kwa vitendo wawapo katika kazi zao za
usafirishaji wa abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es
Salaam. Kiapo hiki kilifanyika mbele ya Kamanda wa kikosi cha Usalama
Barabarani DCP Mpinga wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo kwa madereva wa
Bodaboda Gongolamboto 10/07/2013.
Sehemu
ya Madereva Bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Kamanda wa
Kikosi cha Usalama Barabarani pichani hayupo wakati wa ufungaji wa
mafunzo ya Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Bodaboda. Ufugaji
wa mafunzo hayo ulifanyika Gongolamboto tarehe
0 comments: