HEBU CHEKI MAJINA YA ASILI YA BAADHI YA MASTAR WA BONGO MOVIES HAPA



KWA kawaida binadamu yeyote huzaliwa na kubatizwa jina ambalo hulitumia katika masomo na hata kazi yake.
Tofauti na ilivyo katika fani nyingine, wasanii wamekuwa wakijibatiza majina ya ziada (A.k.a). Mbaya zaidi, majina hayo huwa yanaanza kama utani lakini inafika wakati msanii husika

analizoea jina hilo jipya na kulifanya kuwa kama rasmi. Leo Amani linakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao majina waliyopewa na wazazi wao ‘yamekufa’, hawayatumii kabisa: LULU

Jina lake halisi ni Elizabeth Michael, Lulu lilizoeleka kupitia tasnia ya uigizaji. Alianza kulitumia wakati alipojiunga na Kundi la Sanaa la Kaole.

Hadi leo hii, siyo rahisi kabisa mtu kutokea na kumuita jina la Elizabeth, wengi wanamfahamu kwa jina la Lulu.
RAY
Ray ndiyo jina ambalo limezoeleka na wengi. Vincent Kigosi alilopewa na wazazi wake ni kama limekufa. Kwa zaidi ya miaka kumi sasa tangu alipokuwa kwenye Kundi la Sanaa la Kaole hadi sasa.
Jina la Ray ndiyo watu wanalolifahamu zaidi ingawa hivi karibuni baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa wakijaribu kumuita Vincent ili kurudisha uhai wa jina hilo.






JOHARI
Jina lake halisi ni Blandina Chagula. Johari lilizaliwa kwenye Tamthiliya iliyobeba taito ya jina hilo. Akiwa katika Kundi la Kaole, alianza kujiita Blandy, baadaye alibadilisha jina hilo na kuwa Johari walipoingiza tamthiliya hiyo ambayo pia ilizaa filamu.




“Kuna wakati huwa najuta kutumia jina la a.k.a ambalo limefunika kabisa jina langu la asili,” anasema Johari.

DK. CHENI
Ameanza gemu kitambo, tangu Kundi la Splended. Jina alilopewa na wazazi wake ni Mahsein Awadhi, kwa sasa limekufa. Hakuna anayelitumia, hata yeye mwenyewe.
Jina hilo lilizaliwa baada ya mazoea yake ya kupenda kuvaa cheni kubwa kwenye michezo iliyokuwa ikirushwa Runingani, kwa sasa wengi wanashindwa hata kulitamka jina lake. ODAMA
Jina lake halisi ni Jenniffer Kyaka, limekufa kabisa kwa sasa. Wengi wanamfahamu kama Odama jina ambalo alilipata kwenye filamu iliyoitwa Odama miaka sita iliyopita
Tangu ilipotoka filamu hiyo hadi leo, jina la Odama limegeuka kuwa ndiyo la asili.
BATULI
Jina alilopewa na wazazi wake ni Yobnesh Yusuf lakini wengi hawalijui. Alianzia kuigiza katika Kundi la Kaole. Alianza kujiita Nesh, baadaye akabadilisha na kujiita Batuli baada ya kucheza filamu ya ‘Fake Smile’ ya marehemu Steven Kanumba.
Toka hapo, watu wote wakamfahamu kupitia jina la Batuli, wachache sana wanaolijua jina la Yobnesh, zaidi ni ndugu zake wa karibu.
JB
Majina mengi ya a.k.a ameitwa. Aliitwa Bonge la Bwana, Mtumishi, Eric Ford na mwisho jina la JB likasimama katika akili za watu.
Mwenyewe anasema jina la JB analipenda sana, kuna wakati hata yeye huwa anasahau kabisa kama anaitwa Jacob.



NORA
Jina lake halisi ni Nuru Nassoro. Takriban miaka kumi iliyopita baada ya kujiunga na Kundi la Kaole, jina la Nuru limekufa kabisa.
Familia yake nzima wanatumia jina la Nora na si Nuru tena, amelikubali na analipenda kutoka moyoni mwake.

RICHIE RICHIE
Huyu naye ni msanii wa muda mrefu, jina lake halisi ni Single Mtambalike. Wengi hawalifahamu jina lake halisi.
Wanamuita Richie Richie utadhani ndiyo alilopewa na wazazi wake, jina hilo alipewa takriban miaka kumi na tano iliyopita akiwa na Kundi la Nyota Ensembles.

CATHY
Huyu anaitwa Sabrina Rupia, Cathy lilikuja katika michezo kipindi hicho akiwa katika Kundi la Nyota Ensembles. Limeendelezwa hadi leo na kipo kizazi ambacho hakilifahamu kabisa jina la Sabrina zaidi ya Cathy

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz