MWANAMKE ALIYEBADILI JINSIA NA KUWA MWANAUME AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME...
Mwanaume mmoja aliyebadili jinsia ni wa kwanza barani Ulaya kujifungua mtoto baada ya kuwa mjamzito kwa njia ya kupandikiziwa mbegu za kiume.
Mwanaume huyo ambaye hakutajwa jina, ambaye alizaliwa mwanamke, alijifungua mtoto wa kiume nyumbani kwa msaada wa mkunga katika wilaya masikini ya Neukoellin ya mjini Berlin.
Alisisitiza kujifungulia nyumbani sababu alikataa kuorodheshwa kama mama kwenye nyaraka zozote za hospitali - hitaji la kisheria nchini Ujerumani. Baba huyo, ambaye alibakisha viungo vya uzazi vya mwanamke, amekuwa akifanyiwa tiba za kubadilishwa homoni kwa miaka kadhaa kubadili jinsia.
Habari zaidi kuhusu upandikizwaji mbegu au taarifa za uhusiano wowote zimehifadhiwa kutolewa hadharani kutokana na baba huyo kutaka kumlinda mtoto wake huyo.
Rasmi mtoto huyo, ambaye alizaliwa Machi 18, hana mama, ana baba pekee.
Msemaji wa Mambo na Ndani wa Berlin alisema: "Mtu huyo aliyezusha maswali hakutaka kujitokeza kama mama ila baba kwenye cheti cha kuzaliwa na matakwa hayo yameheshimiwa."
Baba huyo mtarajiwa pia alitaka kwamba jinsia ya mtoto huyo 'isifichuliwe kwa namna yoyote'. Lakini mamlaka zilipuuza hilo na kutangaza kuwa ni wa kiume.
Vyombo vya habari vya Ujerumani viliibuka kwa namna ya kushangaza katika habari ya uzazi huo wa kubadili jinsia.
'Baby belly instead of a beer belly!' (Kitambi mtoto badala ya kitambi bia!") kilikuwa moja ya vichwa vingi vya habari kwenye magazeti ya Ujerumani yakiripoti kuzaliwa kwa mtoto huyo.
Wakati huohuo, Falko Liecke, diwani wa wilaya hiyo ambako mtoto huyo alizaliwa, alisema: "Hiki ni kitu ambacho sikuwahi kusikia maishani ana kushuhudia."
Mwaka 2011 Mahakama Kuu ya Ujerumani iliamuru kwamba mtu binafsi hatakiwi kuondolewa viungo vyake vya uzazi awe mwanamke au mwanaume 'kupata kutambuliwa hadharani kisheria kwa jinsia atakayowekewa'.
Ndio maana baba huyo wa mtoto wa hivi karibuni amekuwa mwanaume wakati akiendelea kuwa na viungo vyake vya uzazi vya kike.
Dk Tobias Pottek wa Hospitali ya Asklepios West mjini Hamburg alisema: "Hata kama mwanamke anataka kuishi kama mwanaume na kuwekewa homoni kuotesha ndevu, kwa kuwa mji wa mimba na mayai bado yapo, pia inawezekana kupata ujauzito.
Hili ni jambo la kwanza la mtoto kuzaliwa barani Ulaya wa mzazi aliyebadili jinsia, lakini katika Marekani jambo la Thomas Beatie, mwanaume aliyebadili jinsia ambaye alikuwa na watoto watatu, linafahamika mno.
Beatie alikuwa akidai talaka kutoka kwa mkewe, lakini alikataliwa sababu jaji hakuweza kuthibitisha kama alikuwa mwanaume wakati akifunga ndoa.
Jaji huyo aliamua hakukuwa na mamlaka ya kisheria ya kuomba talaka kama ndoa hiyo haikuwa ikitambuliwa.
0 comments: