Baada ya kukusanywa maoni ya Katiba,haya ni majumuisho ya maoni hayo.

katibaVugu vugu la Katiba bado linazidi kupamba moto ambapo leo kupitia ukurasa wa Facebook wa Mh. January Makamba amepost kuhusu sehemu na  sehemu ya maoni ambayo amedai ni kwa mujibu wa kitabu cha Takwimu za ukusanyaji maoni ya  katiba.
jKitabu hicho cha Takwimu kimetolewa  na Jaji Joseph Warioba ambae ni Mwenyekiti wa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya.
JOSEPH-SINDE-WARIOBA-TUME-YA-KATIBA-TANZANIA
‘Sehemu ya maoni kwa mujibu wa kitabu cha takwimu za ukusanyaji maoni ya Katiba kama kilivyotolewa na Tume ya Warioba:
Waliotoa maoni: 351,664. Kuhusu muundo wa Muungano: 47,820 au 14%. Serikali 3: 17,783. Serikali 2: 14,234. Serikali 1: 3,674. Mkataba:12,092
Baadhi ya maeneo yaliyoongoza kwa kutolewa maoni: Haki za Binadamu: 13.7%; Muungano: 10.4%; Huduma za Jamii: 8.2%; Urais wa Jamhuri: 7.8%
Katika michango ya haki za binadamu, uhuru wa kuabudu uliongoza kwa 41.5% ya michango ya eneo hili likifuatiwa na suala la ushoga kwa 9.7%
Kwenye michango 105,969 iliyotolewa kuhusu haki za binadamu, haki za wazee zilipata 7.8% ya michango, haki za watoto: 4.4%, wanawake: 5.4%
Maoni 65,535 yalitolewa kuhusu huduma za jamii. Hoja zilizoongoza kwa maoni ni huduma za elimu (75%), afya (14.3%). Huduma nyinginezo (10%).
Kwenye maoni kuhusu elimu,maoni yaliyoongoza ni yale yaliyotaka elimu itolewe bure yakifuatiwa na yale yaliyotaka mfumo wa elimu urekebishwe.
Kwenye maoni yanayohusu huduma za afya, maoni yaliyoongoza (asilimia 28.5) ni yale yanayotaka Serikali igharamie huduma za afya.
Maoni 59,996 yalihusu Urais. 47.7% ya haya, yalihusu Mamlaka ya Rais; 16.7% yalihusu Rais kushtakiwa Mahakamani; 8.3% Rais anavyopatikana.
Katika maoni 28,593 yaliyohusu Mamlaka ya Rais, zaidi ya robo tatu ya maoni (76%) yalitaka mamlaka ya Rais yapunguzwe’.-January Makamba.

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz