HOMA YA NGURUWE YAUA NGURUWE 900 JIJINI MBEYA


Homa ya Nguruwe imerudi tena kwa mara ya pili mkoani Mbeya na kuua zaidi ya nguruwe 900 katika wilaya za Mbeya na Rungwe na kuwaingiza hasara wafugaji wa mifugo hiyo.
Mganga Mkuu wa Mifugo Mkoani Mbeya, Solomon Nong'ona akizungumza na waandishi wa habari leo amesema kuwa ugonjwa huo umerudi tena na kuua zaidi ya nguruwe 900 ambapo ugonjwa huo kwa mara ya kwanza ulizuka mwezi wa Januari.

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz