Kijana akamatwa kwa mauaji London





Shereka Fab-Ann Marsh msichana mwenye umri wa miaka 15 aliyeuawa

Kijana mwenye umri wa miaka 15, amefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji mjini London Uingereza.

Kijana huyo alimuua msichana Shereka Fab-Ann Marsh mwenye umri wa miaka 15 katika mtaa wa Hackney siku ya Jumamosi.

Polisi wamesema kuwa msichana huyo alifariki katika nyumba moja mtaani humo saa kumi Jioni.

Kadhalika Kijana huyo ambaye ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu ya umri wake mdogo, anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Vijana wengine wawili waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo, wameachiliwa na polisi

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz