SHEIKH PONDA ARUDISHWA SEGEREA, MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA DHAMANA YAKE
Ombi la
marejeo lililowasilishwa na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Issa Ponda limetupiliwa mbali na Mahakama Kuu Kanda ya
Dar es Salaam
ilipotoa
uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP), akidai kuwa ombi hilo halikuwa na msingi kisheria.
Kesi hiyo iliyosikilizwa kwa saa 1 na dakika 40 ilitolewa uamuzi na Jaji Augustine Mwarija.
Baada ya uamuzi huo, Sheikh Ponda alirudishwa jela huko Segerea jijini Dar akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi.
Via GPL
0 comments: