Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki shindano la The Voice.
Scuccia aliyeonekana amevalia mavazi yake ya utawa na msalaba shingoni, alijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa kumfikisha katika ushindi huo.
Mtindo wake wa wimbo wa Alicia Keys, kwa jina 'No One', umetizamwa zaidi ya mara milioni 50 katika mtandao wa You Tube tangu auimbe.
Mtawa huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema kuwa aliamua kushiriki mashindano hayo kufuata ushauri wa Papa mtakatifu Francis, kuwa kanisa liwakaribie zaidi watu wa kawaida.