UPDATES KUTOKA MOROGORO: WAKAZI WAANZA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU MANGWEA , TAZAMA PICHA HAPA




 Mama Mzazi wa Mangweha, Denisia Mangweha akiwa nyumbani kwake kabla ya safari kuelekea Uwanja wa Jamhuri.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiwasili nyumbani kwa Mama mzazi wa Mangweha.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera asubuhi hii amefika nyumbani kwa Mama Mangwea eneo la Kihonda Mazimbu Road na kumpa pole kwa niaba ya wakazi wote wa mkoa wa Morogoro. Baada ya kutoa pole, Mhe. Bendera aliongoza umati wa watu kutoka Kihonda kuelekea Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli za kuaga mwili wa Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei 28 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Mangwea anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kihonda nje ya Kanisa la Mtakatifu Monica jirani kabisa na alipozikwa baba yake mzazi Mzee Keneth Mangwea.


 Wakazi wa mjo wa morogoro waanza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu albert Mangwea kabla ya kumpeleka katika Nyumba yake ya Milele. Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala Pema.
 Baadhi ya wasanii na wananchi waliohudhulia uwanjani wakati wa kuaga mwili wa marehemu albert mangwea uwanja wa jamhuri morogoro. 
943280_10152915710755525_916679441_n
Watu wakiaga mwili wa Marehemu albert mangwea uwanja wa Jamhuri morogoro

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz