Unamkumbuka Wabogojo? Sasa anakula show za kimataifa, yupo kisiwa cha mahela, Macau, amshukuru Mr Nice japo alikuwa hampi hela nzuri


Mara ya kwanza kumfahamu Athman Ford "Wabogojo" ni pale nilipotizama video ya wimbo wa Mr Nice  unaoitwa "Kikulacho"...alikuwa anafurahisha sana kwa vitendo vyake ambavyo ni vya kuchekesha na kushangaza kwasababu si kila mmoja wetu anauwezo wa kufanya alichokuwa akikifanya.
Baada ya kuonekana kwenye video hiyo, Wabogojo akaanza kujulikana na hatimae kupata mashafu mpaka nchi za duniani "Europe"
  "Kwaufupi!!Baada ya Ziara ya Europe na Mother africa show ambayo tulipelekwa na Winston Ruddle!! Bwana Winston pia akafanikiwa kutupatia Kazi nyingine ambayo ndio hii ya sasa!!
Mazoezi ya hii shoo tulifanya kuanzia feb 2009 hadi march 2010 pale Belgium Antwerpen Centre baada ya hapo ndio tukaja huku Macau na kuandaa show.
Show tukaanza mwezi 17 Sept 2010 na Mkataba ni Mzuri na Tunalipwa pesa nzuri kwa Mwezi hadi rahaaaa!!Tutakuwa huku hadi Sept 2014 au Zaidi ya hapo inategemea kama utapewa Mkataba Mpya au Kama Umechoka pia ni Uamuzi wako na wao pia!!"

 "Tupo Watanzania 12 katika hii show wengine wote nchi za America,Brazil,Uk,USA NK
Macau ni Kisiwa kipo Asia, Chenye Macasino mengi sanaaa huku watu huja kutumia helaaaa tuuu na Ku gamble, kama Las Vegas USA, na sisi show yetu ipo katika Moja ya Cassino kuuubwa linaitwa CITY OF DREAM na Show yetu yaitwa The House of  Dancing Water."
" Mambo mengi tumejifunza Kuogelea na Scuba Diving pia maana kama hujui kuogelea basi hii show haikufai. 
 Namshukuru Sana Mr Nice japo kuwa hakuwa ananipatia pesa nzuri,Lakini nilichokipata ni zaidi ya pesa!
    Mungu yu mwema!!"

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz