SEREKALI KUPAMBANA NA WACHAFUZI WA MAZINGIRA JIJINI ARUSHA
Wakazi waishio katika kata ya olasiti jijini arusha wameipongeza manispaa ya jiji hilo kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti utupaji wa taka ovyo katika maeneo ya makazi wanapo ishi
Hayo yamesemwa na mmoja wa wakazi hao akifaamika kwa majina ya Jacob marugas alipozungumza na waandishi wa habari kujua mafanikio yaliofikiwa na manispaa ya jiji hilo katika swala la usafi wa mazingira na kujionea mabadiliko makubwa tofauti nahapo awali
Pia ameongeza kuwa swla la magari kupita kila ijumaa saa nne ni tatizo hivyo ombi ni kuongezwa kwa magari nay awe ni yakupita angalau mara tatu katika wiki ili kuepusha tatizo la uchafu kukaa kwa mda mrefu
Hata hivyo wito wake kwa serekali ni manispaa ya jiji la arusha kuongeza idadi ya magari ya kubebea taka pamoja na vitendea kazi kwa wafanya kazi pia ameitaka manispaa hiyo kupanga utaratibu mzuri wa kuwa ni sehemu gani maalumu ya wakzi kukusanya taka ili kuepuka usumbufu wa magari kushindwa kuingia
0 comments: