Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni muigizaji maarufu wa filamu ameanza
kuwa active rasmi kwenye tasnia ya filamu kama mwanzo kwa kuanza
kutengeneza films akiwa kama producer na pia muigizaji kama kawaida.
Lulu kwasasa anashuti filamu ya Mapenzi Ya Mungu akiwa na Mama Kanumba,
Linah na waigizaji wengineo huku yeye akiwa ndiye producer wa filamu
hiyo. Huko nyuma alitengeneza filamu ya Foolish Age ambayo pia
inatarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu na ilichelewa baada ya Lulu
kupata misukosuko kuhusiana na kifo cha Kanumba ambapo pia ilibidi
asicheze filamu kwanza baada ya kuwa segerea kwa miezi kadhaa kabla ya
kupata dhamana
Ukichilia mbali hilo inadaiwa kwasasa baadhi ya waandaji wa filamu
tayari wameanza kumtaka Lulu katika filamu zao baada ya kurudi rasmi
kwenye game kama awali. Lulu ni muigizaji mwenye mashabiki wengi katika
filamu ukiachilia kipaji chake na hivi karibuni alipata tuzo ya
muigizaji bora wa kike kutoka Zanzibar International Film
festival(ZIFF). Hivyo wapenzi wa Lulu kaeni mkao wa kula kuona cheche
zake on screen kama kawaida.
|
|
0 comments: