ROSE NDAUKA SASA KUZAA BILA NDOA,MAMA YAKE AGOMA...
Staa wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa mwezi Aprili, mwakani. Akizungumza na mwanahabari wetu, mchumbaa’ke, Malick Bandawe ambaye ni memba wa kundi la muziki la TNG alianika aya za Kurani kuwa katika Dini ya Kiislamu si ruhusa kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni mjamzito kwani ni sawa na kufunga ndoa na watu wawili hivyo anamsubiri ajifungue kwanza. “Ni kweli mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito na anatarajia kujifungua mapema mwezi wanne, mwakani. “Kuhusu kufunga naye ndoa kwa sasa ni ngumu hadi ajifungue kwani kwa dini yetu (Uislam) si ruhusa kufanya hivyo lakini atakapojifungua tu tutafunga ndoa,” alisema Malick. Malick ambaye hivi sasa anatamba na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema kuwa ana furaha kubwa kuitwa baba mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi Mungu Rose ajifungue salama kwani anampenda kupita maelezo. Baada ya kuzungumza na Malick, gazeti hili lilimtafuta mama wa Rose Ndauka, Batuli kufungukia ishu ya mwanaye kubeba ujauzito kabla ya ndoa ambapo aligoma kuzungumza kwani hakubaliani na suala hilo
0 comments: