WEMA SEPETU AJUTA KUTUMIA MKOROGO, ATAMANI NGOZI YAKE YA AWALI
Wema Sepetu |
kujichubua. Chanzo kimoja makini ambacho kipo karibu na Wema na ambacho pia ni star wa filamu kimeitonya Swahiliworldplanet jana kuwa Wema anajuta kujichubua na hajiamini tena katika urembo tofauti na miaka ya nyuma kwani kila mtu sasa hivi anajua Wema ni fake na amejaa urembo wa kichina kwa aslimia kubwa.
" Wema mliyekuwa mwamjua kwa kujiamini si huyu wa sasa yaani anajuta kutumia mkorogo baada ya kujeruhiwa na madawa hayo yenye sumu, na zile habari kuwa alienda China kuwekwa ngozi ya bandia zilipoenea ndiyo kabisa zikamvunja nguvu, kiufupi Wema anatamani ngozi yake ya mwanzo sababu wengi wanajua urembo wake ni fake, unajua yule amezungukwa na wanafiki wengi wanamsifia hata katika mambo yasiyo na msingi ndiyo sababu akawa anazidisha mkorogo wakati anasifiwa eti mzuri na ana mvuto, sasa yamemtokea na puani... mimi akhaa! siwezi kuingia kwenye mkumbo huo" kilisema chanzo hicho
0 comments: