Bob Junior adai kutosikilizwa na vyombo vya dola pale anaposhtaki udhalilishaji anaofanyiwa na magazeti ya udaku
Kufuatia kuandamwa na magazeti ya udaku, Rais wa Masharobaro na
hitmaker wa Bashasha, Raheem Ramadhani a.k.a BOB JUNIOR amesema kuwa
licha ya kuandikwa vibaya kwa kile alichokidai kuwa ni udhalilishaji
dhidi yake, amekuwa akienda kushitaki kwenye vyombo vya dola lakini
hasikilizwi.
Bob Junior amesema kutokana na kutosikilizwa amekuwa akikosa njia mbadala yakupata haki yake.
“Hata ukitaka kuweza kushitaki hausikilizwi yaani hata haieleweki
haileweki yaani wee acha tu(kwa msisitizo), mengi siku zote magazeti
yamekuwa yananiandika tu hovyo… hovyo… hovyo… hata sijui wanajiandikia
tu. Wewe angalia hata magazeti ya Kiu utaona, magazeti ya wiki iliyopita
wamenichoresha mimi siku zote,” Bob Junior alikiambia kipengele cha
Chumba Cha Sindano cha kipindi cha Kali za Bomba cha Bomba FM, Mbeya.
Akielezea sababu za kuandamwa yeye tu na si msanii mwingine, Bob
Junior alisema: Aaaah bwana wee unajua mtu ukishakuwa juu umenielewa
bwana! wewe angalia mtu yeyote yaani akishakuwa juu tu yaani ndio
inavyokuwa wenyewe ndio wanaona sijui ni biashara kwao, wanaweza
kutafuta vistori vingine vinahusiana na ukweli vingine vya uongo basi
hizo za uongo wataziandia sana wataziforce ziwe za ukweli.”
Source: Bongo5
0 comments: