Kipenga cha kumrithi Mgimwa chapulizwa





Msafara wa Tendega ulianza majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Igumbilo umbali wa Kilomita saba katikati ya Mji wa Iringa.PICHA|MAKTABA


Katika kile kilichotafisriwa kama kuvurugu shamramshara zilizoandaliwa na Chadema Nyanda za Juu Kusini, Mkoa wa Iringa Wilaya na Jimbo, polisi waliibuka katika eneo la Mlima Ipogolo na kuzuia msafara.

Iringa.Mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega jana alichukua kwa mbwembwe fomu ya kuwania kiti hicho, huku msafara wenye magari na pikipiki ukizuiwa na polisi mkoani hapa kwa madai ya kutokuwa na ruhusa.


Msafara wa Tendega ulianza majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Igumbilo umbali wa Kilomita saba katikati ya Mji wa Iringa.


Mpaka unazuiwa, msafara huo uliokuwa ukiuongozwa na pikipiki zaidi ya 50, magari zaidi ya 10 ulikuwa umetembea kilomita tano na ulizuiwa wakati wanachama hao walipokuwa wakipandisha mlima wa Ipogolo.


Katika kile kilichotafisriwa kama kuvurugu shamramshara zilizoandaliwa na Chadema Nyanda za Juu Kusini, Mkoa wa Iringa Wilaya na Jimbo, polisi waliibuka katika eneo la Mlima Ipogolo na kuzuia msafara.


Baada ya majadilino ya dakika 20, polisi waliruhusu gari ya mgombea kupita na kuelekea ziliko Ofisi za Tume kwa ajili ya kuchukua fumo na kusisitiza kuwa wasingeruhusu magari mengine na pikipiki kumsindikiza.


Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Grace aliwataka wananchi wa Iringa kutohofia vitendo vilivyofanywa na Jeshi la Polisi ikiwamo ya kuzuia msafara wake wakati akichukua fomu, bali wanapaswa kutambua kuwa huo ni mwanzo tu wa harakati za ukombozi.

0 comments:

Copyright © 2012 KARINGA NEWS Tz